Sunday 28 February 2010

Man United Mabingwa!!!!
Aston Villa 1 Man United 2
Wayne Rooney, alieanza benchi na kuingizwa kumbadilisha Michael Owen alieumia dakika ya 42, ndie aliewapa kikombe Manchester United kwa kufunga bao la pili na kuwang’oa Aston Villa kwa bao 2-1 na kutwaa Kombe la Carling leo Uwanjani Wembley Jijini London.
Hiii ni mara ya pili mfululizo kwa Manchester United kutwaa Kombe hilo baada ya kushinda msimu uliokwisha kwa kuwabwaga Tottenham Fainali.
Aston Villa ndio waliokuwa wa kwanza kufunga pale walipopewa penalti dakika ya 5 tu ya mchezo baada ya Beki wa Man United Nemanja Vidic kumchezea rafu Gabriel Agbonlahor na Refa Phil Dowd kutoa penalti iliyofungwa na James Milner.
Michael Owen aliisawazishia Man United dakika ya 12 baada ya upiganaji mzuri wa Dimitar Berbatov.
Owen akaumia dakika ya 42 na kutoka na nafasi yake kushikwa na Wayne Rooney.
Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1.
Kipindi cha pili, dakika ya 74, gonga safi kati ya Berbatov na Valencia, Mchezaji aliepewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi, ilimaliziwa na krosi murua ya Valencia na Rooney akajitwisha na kufunga kwa kichwa safi.
Rooney alikosa kufunga bao la 3 pale kichwa chake kufuatia krosi ya Valencia kupiga posti huku Kipa wa Villa Brad Friedel akigalagala.
Vikosi vilivyoanza:
Aston Villa: Friedel, Cuellar, Collins, Dunne, Warnock, Ashley Young, Milner, Petrov, Downing, Heskey, Agbonlahor.
Akiba: Guzan, Luke Young, Sidwell, Carew, Delfouneso, Delph, Beye.
Man Utd: Kuszczak, Rafael Da Silva, Vidic, J Evans, Evra, Valencia, Fletcher, Carrick, Park, Owen, Berbatov.
Akiba: Foster, Neville, Brown, Rooney, Scholes, Gibson, Diouf.
Refa: Phil Dowd
LIGI KUU:
Liverpool 2 Blackburn Rovers 1
Uwanjani Anfield, Liverpool walipata ushindi wa 2-1 mbele ya Blackburn kwenye mechi ya Ligi Kuu na sasa wapo nafasi ya 6 kwenye Ligi wakiwa na pointi 48 kwa mechi 28 wakiwa pointi moja tu nyuma ya Tottenham na Man City zilizofungana kwa pointi ingawa Tottenham yuko juu kwa magoli lakini Man City wana mechi moja pungufu.
Liverpool walipata bao la kwanza dakika ya 20 kupitia Steven Gerrard na Blackburn wasawazisha dakika ya 40 kwa penalti iliyopigwa na Keith Andrews baada ya Jamie Carragher kushika mpira.
Fernando Torres akawapa ushindi Liverpool kwa kufunga bao la pili dakika ya 44.
Sunderland 0 Fulham 0
Ndani ya Stadium of Light, Sunderland wameshindwa kupata ushindi na kwenda sare ya 0-0 na Fulham katika mechi ya Ligi Kuu hii ikiwa ni mechi ya 14 kwa Sunderland bila ushindi.
Mechi ya mwisho Sunderland kuonja ushindi ni Novemba mwaka jana walipoifunga Arsenal.

No comments:

Powered By Blogger