Wednesday 3 March 2010

Ireland 0 Brazil 2
Bao la kujifunga wenyewe Ireland kwenye dakika ya 44 baada ya krosi ya Robinho kumgonga Kevin Doyle na kuingia na lile la Robinho la dakika ya 76, liliwapa ushindi Brazil wa 2-0 juu ya Ireland ndani ya Uwanja wa Emirates Jijini London hapo jana Jumanne usiku katika mechi ya kirafiki.
Brazil walitawala na kucheza vizuri sana Kipindi cha Pili na bao lao la pili la Robinho lilifungwa baada ya pasi zao 22 na Getafe kumpasia kwa kisigino Robinho alieupindisha mpira wavuni.
Bila shaka, uchezaji wa Timu ya Brazil utamfurahisha sana Kocha wao Dunga kwani walicheza kwa kiwango cha kuridhisha na hayo ni mazoezi tosha kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Brazil wataanza kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini hapo Juni 15 kwa mechi dhidi ya Korea Kaskazini huko johannesburg.
Vikosi vilivyoanza:
Ireland: Shay Givens, Kelly, St. Ledger, McShane, Kilbane, Lawrence, Whelan, Keith Andrews, Duff, Kevin Doyle, Robbie Keane.
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos, Ramires, Silva, Felipe Melo, Kaka, Adriano, Robinho

No comments:

Powered By Blogger