Monday 1 March 2010

Zidane kamwe kumtaka radhi Materazzi!!
Supastaa wa Ufaransa Zinedine Zidane amesema ni heri kufa kuliko kumwomba radhi Marco Materazzi kwa kichwa alichomtwisha kwenye Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
Zidane, kwenye Fainali hiyo ikiwa ni mechi yake ya mwisho kabla kustaafu, alimpiga kichwa Materazzi kwenye muda wa nyongeza wa Fainali ambayo baadae Italia walinyakua Ubingwa wa Dunia kwa kushinda mikwaju ya penalti.
Zidane amekiri kujutia kitendo chake lakini hawezi kuomba radhi kwa vile Materazzi alimtukania Mama yake.
Zidane amesema: “Najuta! Lakini nikiomba radhi ni sawa na kukubali walichofanya ni sawa. Wakati huo Mama yangu alikuwa mgonjwa. Alikuwa hospitali. Ulikuwa wakati mbaya kwangu. Ingekuwa kitendo kile kafanya Kaka, ambae ni muungwana, ningeomba radhi! Lakini huyu, ntakuwa najikosea heshima mwenyewe!”
Wenger aomba kuumia Ramsey kusilete dosari
Arsenae Wenger anaomba sana kuumia vibaya kwa Kijana Aaron Ramsey katika mechi ya Ligi Kuu na Stoke City siku ya Jumamosi kusije kukaleta madhara kwa Wachezaji wake na kuwaathiri kisaikolojia.
Ramsey alivunjwa vibaya mguu na Mchezaji wa Stoke Ryan Shawcross ambae alipewa Kadi Nyekundu.
Kuumia huko kwa Ramsey kumemkasirisha Wenger ambae amedai Timu yake yenye Wachezaji wengi Chipukizi hukamiwa na kuchezewa undava na kuumizwa.
Ramsey alipelekwa hospitali na kufanyiwa operesheni na Madaktari wamesema wanategemea atapona vizuri.
Arsenal wameshawahi kuumiziwa Wachezaji wao vibaya kwa rafu mbaya ambazo ziliwaumiza Abou Diaby na hasa Eduardo ambae alikaa muda mrefu nje ya Uwanja baada ya kuumizwa na kuvunjwa enka.
Wenger anasema: “Katika Kiungo tuna Wachezaji kama Fabregas, Nasri na Eboue ambao wastani wa umri wao ni miaka 21 tu! Mbele yupo Bendtner, ana miaka 20 tu! Wachezaji wazuri sana lakini unawateketeza kwa kuwajeruhi! Hawatakuwa Wachezaji tena! Hii ni kashfa!”

No comments:

Powered By Blogger