Monday 1 March 2010

Fergie abeba Kikombe cha 34!!!
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson jana alinyakua Kikombe chake cha 34 tangu atue Manchester United baada ya Timu yake kuipiga Aston Villa 2-1 na kutwaa Kombe la Carling Uwanjani Wembley.
Bao la ushindi la Manchester United lilifungwa na Wayne Rooney dakika ya 74 katika mechi ambayo Aston Villa ndio walioanza kufunga dakika ya 3 tu ya mchezo walipopewa penalti baada ya Nemanja Vidic kumvuta jezi Gabriel Agbonlahor kitendo ambacho Meneja wa Aston Villa Martin O’Neill amedai kilistahili Kadi Nyekundu.
Hata hivyo, Michael Owen aliisawazishia Man United bao dakika ya 12 ya mchezo.
Kuhusu faulo ya Vidic kwa Agbonlahor, Ferguson alisema walibahatika sana kwa Vidic kutopewa Kadi yeyote na Refa Phil Dowd.
Ingawa Martin O’Neill alitaka Vidic atolewe, Nahodha wake Richard Dunne amesema haoni kama ingewasaidia endapo Man United wangecheza mtu 10 kwani katika mechi ya Ligi Kuu hivi karibuni Man United walicheza mtu 10 na Villa baada ya Winga Nani kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa zaidi ya saa nzima na wakacheza vizuri sana na kupata sare ya 1-1 nyumbani kwa Villa.
KWINGINEKO ULAYA: Matokeo
BUNDESLIGA
Jumapili, Februari 28
Hannover 0 Wolfsburg 1
Bayern Munich 1 Hamburg 0
LA LIGA
Jumapili, Februari 28
Xerez 1 Espanyol 1
Villareal 1 Deportivo la Coruna 0
Sporting Gijon 3 Osasuna 2
SERIE A
Jumapili, Februari 28
Napoli 2 AS Roma 2
Genoa 3 Bologna 4
Juventus 0 Palermo 2
Parma 1 Sampdoria 0
AC Milan 3 Atalanta 1
Udinese 2 inter milan 3
Livorno 1 Siena 2
Chievo 2 Cagliari 1

No comments:

Powered By Blogger