Sunday 28 February 2010

Kikosi cha England hadharani!!
• Aliemvunja Ramsey yumo Kikosini!
Fabio Capello amekitaja Kikosi cha England kitakachocheza mechi ya kirafiki na Misri hapo Jumatano Uwanjani Wembley na Kikosini yumo Mchezaji wa Stoke City Ryan Shawcross aliemvunja mguu Aaron Ramsey wa Arsenal hapo jana Timu hizo zilipocheza kwenye Ligi Kuu.
Kikosi kamili: James (Portsmouth), Green (West Ham), Hart (Birmingham), Brown (Man Utd), Terry (Chelsea), Upson (West Ham), Lescott (Man City), Shawcross (Stoke), Baines (Everton), Warnock (Aston Villa), Milner (Aston Villa), Beckham (AC Milan), Walcott (Arsenal), Lampard (Chelsea), Barry (Man City), Gerrard (Liverpool), Carrick (Man Utd), Wright-Phillips (Man City), Downing (Aston Villa), Heskey (Aston Villa), Defoe (Tottenham), Rooney (Man Utd), Crouch (Tottenham), Carlton Cole (West Ham).
Stoke 1 Arsenal 3
• Ushindi waingia doa kwa kuumia vibaya Ramsey!
Jana kwenye Uwanja wa Britannia Arsenal ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stoke City kwenye Ligi Kuu na kufikisha pointi 58 wakiwa nafasi ya 3 huku juu yao wapo Manchester United wenye pointi 60 na vinara Chelsea wenye pointi 61.
Ushindi huo wa Arsenal umeingia dosari kubwa kwa kuumia vibaya kwa Mchezaji wao Chipukizi Aaron Ramsey alievunjwa mguu na Mchezaji wa Stoke Ryan Shawcross aliepewa moja kwa moja Kadi Nyekundu.
Kuumia kwa Ramsey kunafanana na kuumia kwa Mchezaji mwingine wa Arsenal Eduardo alieuvunjwa na Martin Taylor wa Birmingham miaka miwili iliyopita.
Ramsey alifanyiwa upasuaji na atakuwa nje msimu wote.

No comments:

Powered By Blogger