Wednesday 3 March 2010

Leo England v Misri, Wembley Stadium
England leo saa 5 usiku saa za bongo itakwaana na Mabingwa wa Afrika kwa mara 3 mfululizo, Misri, Uwanjani Wembley, Jijini London.
Ingawa pambano hili ni mechi ya kirafiki lakini kwa England limekuwa likitangazwa kwa sababu zisizohusu mechi hii kutokana na skandali la aliekuwa Nahodha wa England, John Terry, ambae amekumbwa na kashafa ya kutembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge.
Kashfa hiyo ikasababisha John Terry kutemwa Unahodha wa England na Wayne Bridge kugoma kuichezea England ili asikutane na Terry kwenye Kikosi hicho.
Misri imechaguliwa kuipa mazoezi England hasa kwa vile kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, England iko Kundi moja na Algeria, Timu ambayo iliibwaga Misri nje ya Fainali za Kombe la Dunia.
Kocha wa Misri, Hassan Shehata, amesema ingawa England ina Wachezaji wazuri sana wao hawaihofii na England isiwadharau wao.
Vikosi vinategemewa kuwa:
England: Hart, Brown, Terry, Upson, Baines, Lampard, Barry, Walcott, Gerrard, Rooney, Heskey.
Egypt: El Hadary, Fathi, Gomaa, Said, Nagy, Abd Rabo, Hassan, Ghaly, Moawad, Zidan, Moteab.
Rio aliona yeye ni Kepteni England kwenye TV!!
Rio Ferdinand amekiri kuwa hakuambiwa yeye ndie Kepteni mpya wa England na badala yake aliona tu taarifa kwenye TV.
Mwezi uliokwisha, aliekuwa Nahodha wa England, John Terry, alipokonywa Ukepteni baada ya kuibuka skandali kuwa ametembea na gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge.
Rio Ferdinand ndie alikuwa Makamu Kepteni wa England na Kocha wa England, Fabio Capello, alimthibitisha Rio ndie Kepteni mpya baada ya Terry kuvuliwa madaraka hayo.
Hata hivyo, Rio amesema hajaongea lolote na Capello na Kocha huyo hajaieleza chochote Timu ya England.
Pia Rio Ferdinand amemsifia Capello na kumfananisha na sir Alex Ferguson, Meneja wa Klabu yake, Manchester United, kwa umahiri, umakini wa kazi yake na kuwa mkweli.
Bongo 2 Uganda 3
Katika mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Tanzania, na Uganda iliyochezwa leo jioni, Tanzania imebwagwa kwa bao 3-2.

No comments:

Powered By Blogger