Tuesday 12 August 2008


ASTON VILLA WAMCHUKUA MHISPANIA KUTOKA RANGERS
Klabu ya LIGI KUU UINGEREZA Aston Villa imemnunua Mlinzi Carlos Cuellar [26] kutoka Klabu ya Rangers ya Scotland kwa bei ya Pauni milioni 7.8.
Cuellar alikwenda Rangers mwaka jana akitokea Klabu ya Spain Osasuna na alikuwa moja ya nguzo thabiti kwa Rangers na kuuzwa kwake kumekuja kwa mshangao wa wadau wengi.
Cuellar ni mchezaji wa 6 kusainiwa na Aston Villa msimu huu.
Wengine ni Curtis Davies, Steve Sidwell, Luke Young, Nicky Shorey na Kipa Brad Friedel.
TOTTENHAM WAMNUNUA KIPA KUTOKA SPAIN
Tottenham wamethibitisha wamemnunua Kipa veterani Cesar Sanchez [36] kutoka klabu ya Spain Real Zaragoza na anategemewa kuwa Kipa namba mbili wa timu hiyo.
Kipa namba moja atakuwa Heurelho Gomes aliechukuliwa kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi kuziba pengo lililoachwa na kipa wa zamani wa Uingereza Paul Robinson aliehamia Blackburn Rovers.
Meneja wa Tottenham Spurs kwa sasa anafanya ‘mapinduzi’ klabuni hapo baada ya kuwauza wachezaji kadhaa wakiwemo Robbie Keane alieenda Liverpool, Steed Malbranque, Pascal Chimbonda, Teemu Tainio na Younes Kaboul.
Wachezaji walionunuliwa ni John Bostock (Crystal Palace, £700,000), Heurelho Gomes (PSV Eindhoven), Luka Modric (£15.8m), Giovani dos Santos (Barcelona, £4.7m) na David Bentley (Blackburn, £15m).

No comments:

Powered By Blogger