Saturday 16 August 2008

SASA BENCHI LA AKIBA KUWA NA WACHEZAJI 7
LIGI KUU UINGEREZA imetoa uamuzi wa kuruhusu kila timu kuwa na Wachezaji 7 wa Akiba kwenye benchi la akiba la mechi za LIGI KUU kwa msimu huu wa 2008/9. Mtindo huu pia unatumika kwenye mechi zote za UEFA. Hapo nyuma kila timu iliruhusiwa kuwa na wachezaji watano tu wa akiba.
Lakini ingawa kila timu itakuwa na Wachezaji 7 wa Akiba kwenye benchi, timu inaruhusiwa kubadilisha si zaidi ya Wachezaji watatu katika kila mechi kama ilivyokuwa misimu iliyopita.
Mameneja wengi wa Timu za LIGI KUU wameusifia uamuzi huu kwani unawapa fursa kuwaweka wachezaji wao wadogo na chipukizi kwenye listi ya timu na pengine kuwatumia katika mechi na kuwapa uzoefu kwani wanaweza kuwaingiza ikiwa timu yao inafanya vizuri kwenye mechi mathalani timu inaongoza mabao 3-0 na dakika zimebaki labda 10 hivi basi ni rahisa kumuingiza chipukizi ili apate uzoefu. Awali timu zilikuwa zinaogopa kuwaweka chipukizi kwenye benchi la akiba kutokana na idadi ndogo ya Wachezaji wa Akiba wanaoruhusiwa na wasiwasi wa timu kujihujumu ikiwa mechi inaenda kombo. Hivyo timu zilihakikisha benchi la akiba lina Wachezaji watano mahiri na hivyo kuwakosesha chipukizi nafasi ya kucheza katika mechi ambazo zinageuka kuwa rahisi.
KIKOSI CHA MAN U NA NAMBA ZAO ZA JEZI
Kikosi cha Manchester United cha msimu wa 2008/9 kimewasilishwa rasmi kwenye LIGI KUU UINGEREZA huku kila Mchezaji akiwa na namba yake maalum atakayokuwa akiitumia kwenye jezi akicheza mechi.
Kikosi hicho kina Wachezaji wapya kama Mapacha wa Kibrazil Fabio na Rafael Da Silva pamoja na chipukizi wengine kama Danny Welbeck, Federico Macheda, Gibson, Campbell, Cleverley, Gray, Cathcart, Zieler, Chester na Kipa Amos.
Pia yumo Mshambuliaji hatari wa Angola aitwae Manucho ambae kwa sasa yuko mbioni kuombewa kibali cha kuishi Uingereza.

LISTI KAMILI NA NAMBA ZA JEZI NI KAMA IFUATAVYO:
1.Van der Sar, 2.Neville, 3.Evra, 4.Hargreaves, 5.Ferdinand, 6.Brown, 7.Ronaldo, 8.Anderson, 9.Saha, 10.Rooney, 11.Giggs, 12.Foster, 13.Park, 15.Vidic, 16.Carrick, 17.Nani, 18.Scholes, 19.Welbeck, 20.Fabio, 21.Rafael, 22.O'Shea, 23.Evans, 24.Fletcher, 26.Manucho, 27.Silvestre, 28.Gibson, 29.Kuszczak, 31.Campbell, 32.Tevez, 33.Hewson, 34.Possebon, 35.Cleverley, 36.Gray, 37.Cathcart, 38.Zieler, 39.Chester, 40.Amos, 41.Macheda

No comments:

Powered By Blogger