Friday 15 August 2008


MSIMU KUANZA KESHO!!!
Msimu mpya wa LIGI KUU UINGEREZA unaanza rasmi kesho Jumamosi miezi mitatu baada ya Manchester United kuchukua Ubingwa kwa mara ya 10 kwa mechi itakayoaanza saa 8 dakika 45 mchana kwa saa za bongo kati ya Arsenal na timu iliyopanda daraja West Bromwich Albion. Timu nyingine zilizopanda daraja na ambazo pia zitacheza kesho hiyo ni Stoke City na Hull City. Stoke watacheza na Bolton na Hull City watakwaana na Fulham.
Mabingwa Man U na washindi wa pili Chelsea wataanza kampeni Jumapili. Man U watawakaribisha Newcastle na Chelsea watakuwa wenyeji wa Mabingwa wa Kombe la FA Portsmouth.
Wakati Man U hawajamnunua mchezaji yeyote mpaka sasa ingawa muda wa usajili bado na mwisho wake ni tarehe 31 Agosti 2008, Chelsea washawabeba Wareno Deco na Bosingwa huku Arsenal wana wawili wapya Mfaransa Samir Nasri na tineja Aaron Ramsey. Liverpool wamemchukua mfungaji Robbie Keane.
Mabingwa Man U watauanza msimu bila ya mchezaji wao ambae ni Mfungaji na Mchezaji Bora wa msimu uliopita Cristiano Ronaldo anaeuguza enka aliyofanyiwa operesheni.
Timu zilizoshuka daraja msimu uliopita ni Derby,Birmingham na Reading.
Msimu huu mpya wadau wengi wanategemea bingwa atatoka kati ya timu zilizomaliza nafasi nne za juu msimu uliopita yaani Man U, Chelsea, Liverpool au Arsenal zinazoongozwa na Mameneja Sir Alex Ferguson, Scolari, Wenger na Benitez.
Chelsea alichukua ubingwa mara ya mwisho miaka miwili iliyopita. Liverpool hajatwaa ubingwa tangu 1990 na Arsenal tangu 2004.


JUMAMOSI 16 August 2008
[MECHI ITAANZA SAA 11 JIONI SAA ZA BONGO LABDA ITAJWE TOFAUTI]
Arsenal v West Brom [SAA 8 DAK 45 MCHANA]
Bolton v Stoke
Everton v Blackburn
Hull v Fulham
Middlesbrough v Tottenham
Sunderland v Liverpool [SAA 1 NA NUSU USIKU]
West Ham v Wigan

JUMAPILI 17 August 2008
Aston Villa v Man City [SAA 11 JIONI]
Chelsea v Portsmouth [SAA 9 NA NUSU]
Man Utd v Newcastle [SAA 12 JIONI
]

No comments:

Powered By Blogger