Friday, 15 August 2008

NEWCASTLE WAIMARISHA NGOME!
Newcastle wamethibitisha kumsaini Mlinzi wa Deportivo La Coruna Muargentina Fabricio Coloccini kwa mkataba wa miaka mitano.
Coloccini atakuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na Meneja Kevin Keegan wengine wakiwa ni Danny Guthrie na Jonas Gutierrez.
Coloccini ni mlinzi mwenye nguvu alieanza kandanda akiwa na Klabu ya Argentina Boca Juniors na baadae akahamia Italia kuchezea AC Milan.
Kisha akatangatanga Klabu za Spain zikiwemo San Lorenzo, Alaves, Atletico Madrid na Villarreal.
Januari 2005 alijiunga na Deportivo La Coruna.
Coloccini ameshachezea Timu ya Taifa ya Argentina na mwaka 2006 alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye Kombe la Dunia walipotolewa na wenyeji wa mashindano hayo Ujerumani.
....................MAN CITY WADODA NYUMBANI!!!
Manchester City jana wameadhiriwa vibaya nyumbani kwao baada ya kuchapwa bao 1-0 na timu hafifu ya Denmark FC Midtjylland katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la UEFA.
Timu hiyo ya Denmark ilifunga bao la la ushindi kupitia Danny Olsen dakika ya 15 baada ya kosa la mlinzi Richard Dunne.
Timu hizi zitarudiana huko Denmark baada ya wiki mbili.
...................ASTON VILLA WAPETA UGENINI!!
Wakati Manchester City wakila kibano, mchezaji Gareth Barry ambae wengi wanategemea yuko njiani kwenda Liverpool msimu huu aliifungia Aston Villa bao moja katika dakika ya 4 kwenye mechi ya Kombe la UEFA waliyocheza ugenini huko Iceland dhidi ya FH Hafnarfjordur na kushinda mabao 4-1.
Mabao mengine ya Aston Villa yalifungwa na Ashley Young ,dakika ya 6, Agbonlahor [38] na Laursen [64].
..................PORTSMOUTH WASHTAKIWA!!!
Portsmouth wameshitakiwa na Chama cha Soka Uingereza FA kwa kuvunja kanuni za uhamishaji Wachezaji kuhusiana na uhamisho wa Mchezaji wa Zimbabwe Benjani Mwaruwaru wakati alipojiunga na Portsmouth Januari 2006 akitokea Klabu ya Auxerre ya Ufarnsa na pale alipohama Portsmouth Januari 2008 kwenda Manchester City.
Utata wa uhamisho wa Benjani hasa unamuhusu ajenti wa Benjani aitwae Willie McKay ambae nae anahusishwa kwenye mashtaka hayo.
Sheria za FA zinakataza maajenti kuhusika na Klabu mbili katika uhamisho wa mara mbili mfululizo unaohusu mchezaji mmoja.
Portsmouth wanatakiwa kuwasilisha utetezi kabla ya Agosti 29, 2008 ingawa tayari wameshakana tuhuma hizo kwa kusema hawakumlipa Ajenti yeyote Benjani alipojiunga na Portsmouth Januari 2006 akitokea Klabu ya Auxerre na uhamisho wake kwenda Manchester City ulibarikiwa na LIGI KUU UINGEREZA pamoja na Kamati husika ya FA.


No comments:

Powered By Blogger