Tuesday 22 December 2009

Meneja Mpya Man City atangaza Ubingwa ndani ya Miezi 18!!!
Baada ya kutambulishwa hapo jana, Mtaliana Roberto Mancini aliechukua nafasi ya Umeneja Manchester City iliyokuwa ya Mark Hughes aliefukuzwa Jumamosi iliyopita, amejigamba kuwa atachukua Ubingwa wa England ndani ya kipindi cha Miezi 18.
Mancini, aliewahi kuwa Meneja wa Inter Milan huko Italia, atasaidiwa na Meneja Msaidizi Brian Kidd aliewahi kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Manchester United.
Mara baada ya utambulisho, Mancini akajigamba: “Kwa sasa tunalenga kumaliza Ligi Kuu tukiwa ndani ya Timu Bora Nne. Msimu ujao, tunataka tuchukue Ubingwa!”
Wakati huohuo, Mark Hughes, aliemwaga unga Man Cuty, amelalamika kuwa hakupewa taarifa mapema kuwa ataondolewa lakini mrithi wake alikuwa tayari ameshatayarishwa na hivyo kuthibitisha kulikuwa na mipango ya muda mrefu kumwondoa.
Hughes amelalamika kuwa malengo waliyokubaliana na Wamiliki wa Man City ambao ni Koo ya Kitajiri ya Kifalme toka Abu Dhabi yalikuwa ni kuumaliza msimu huu wa Ligi Kuu England wakiwa katika Timu 6 Bora kitu ambacho kilikuwa kinawezekana kwani Timu imepoteza mechi 2 tu ikiwa ni idadi ndogo kupita Timu zote Ligi Kuu.
Hata hivyo Man City imetoka sare mechi 8 zikiwa ni nyingi mno na wameshinda mechi 7 na wako nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu.
Messi Mchezaji Bora Duniani 2009!!
Ronaldo Mfungaji wa Goli la Mwaka!!!
Marta ni Bora kwa Mabibi!!!
Nyota wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi, miaka 22, ametunukiwa Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora kwa Mwaka 2009.
Messi pia hivi karibuni alishinda Tuzo maarufu ya Ballon d’Or ikiashiria ni Mchezaji Bora Ulaya.
Mshindi wa Mwaka jana, Cristiano Ronaldo, amekuwa Mshindi wa Pili.
Kwa upande wa Wanawake, Marta wa Brazil, ndie Mchezaji Bora 2009 ikiwa ni mara yake ya nne mfululizo kutwaa Tuzo hiyo.
Katika sherehe zilizofanyika Zurich, Uswisi hapo jana, Messi alitamka: “Tafadhali, mie si Mfalme wa Dunia wala si nambari wani duniani! Siamini vitu hivyo!!! Nimebahatika tu kuchezea Timu nzuri Barca!!!”
Cristiano Ronaldo alipewa Tuzo ya FIFA iliyokuwa ikitolewa kwa mara ya kwanza iitwayo Puskas [Hili ni jina la Mchezaji Nyota wa zamani toka Hungary] kwa kufunga Goli Bora la Mwaka. Goli lililompa Tuzo hiyo ni lile alilofunga akiwa na Manchester United mwezi Aprili 2009 kwenye mechi ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE alipopiga mkwaju toka Mita 40 na kuwafungA FC Porto.
FIFA pia ilitangaza Majina ya Wachezaji Bora 11 wanaounda Kikosi Bora nao ni: Kipa: Casillas, Mabeki: Dani Alves, Evra, Vidic, Terry, Viungo: Xavi, Iniesta, Gerrard Mastraika: Ronaldo, Messi na Torres.

No comments:

Powered By Blogger