Thursday, 29 October 2009

Larsson astaafu Soka huku akimwaga machozi!!!
Henrik Larsson amestaafu kucheza soka ya kulipwa mara baada ya kuichezea Klabu ya Helsingborg ya Sweden ambayo ipo mji aliozaliwa ilipokuwa ikicheza na Djurgarden na kufungwa 2-0.
Larsson, umri miaka 38, alianza soka akichezea Klabu ya Hogaborg kisha Helsingborg, Feyernoord, Celtic, Barcelona na Manchester United na kufunga jumla ya mabao 415.
Larsson pia ameichezea Timu ya Taifa ya Sweden mara 100 na kufunga mabao 37.
Mshambuliaji Nyota huyu ameshashinda Ubingwa wa Scotland mara 4 akiwa na Celtic, Ubingwa wa Spain mara 2 na Barcelona na pia UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Barca mwaka 2006.
Alipokuwa na Manchester United aliisaidia klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa England.
Mara baada ya mechi yake hiyo ya mwisho skrini kubwa hapo uwanjani ziliwaonyesha Sir Alex Ferguson, Meneja wa zamani wa Sweden Lars Lagerback na Mchezaji Zlatan Ibrahimovich wakitoa pongezi zao kwa Larsson kwa mafanikio yake kati historia yake ya Uchezaji na hilo lilimfanya Henrik Larsson alengwe na machozi.
Klabu yake ya Helsingborg imeamua kuistaafisha jezi namba 17 aliyokuwa akiivaa Larsson.
Mchezaji wa Ligi Kuu Lupango Miezi 18!!!!
Klabu yake Wigan yamfukuza!!!!
Marlon King, umri miaka 29 na Raia wa Jamaica anaechezea Wigan, amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kumshambulia na kumvunja pua Mwanamke wa miaka 20 kwenye baa.
Tukio hilo lilitokea Desemba mwaka jana na leo ndio ilikuwa hukumu ya kesi yake.
Mara baada ya hukumu, Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan ametangaza kuwa Mchezaji huyo atafukuzwa moja kwa moja mara baada ya notisi kwake ya siku 14 kumalizika.
Whelan ametamka: “Hana nafasi hapa! Hatukubali uhuni huo!”

No comments:

Powered By Blogger