Thursday 29 October 2009

Martinez ampigia simu Ferguson kujieleza!
Meneja wa Wigan Roberto Martinez amempigia simu Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ili kukanusha taarifa zilizozagaa hapo jana kuwa alitamka Ferguson anaogopewa na FA na pia anasaidiwa na Mameneja wengine wa Klabu za Ligi Kuu, hasa Steve Bruce na Sam Allardyce, ili kumsakama Mhispania mwenzake Rafa Benitez ambae ni Meneja wa Liverpool.
Martinez vilevile amewapigia simu Steve Bruce na Sam Allardyce kukanusha taarifa hizo na kujieleza zaidi binafsi kwao.
Inasemekana taarifa za hayo madai ya Martinez chanzo chake ni Vyombo vya Habari vya Spain.
Martinez, mwenye umri wa miaka 36, amesema: “Ni bahati mbaya lakini watu lazima wanielewe! Mimi siwezi kuwasema hao Mameneja wenzangu! Kwanza mie ni mdogo, sijashinda Ligi! Sir Alex ni Meneja Bora Duniani! Steve Bruce nina uhusiano mzuri nae na alikuwa hapa Wigan kabla yangu! Na naheshimu mafanikio ya Allardyce kwenye Ligi Kuu!”
Martinez vilevile amekijulisha Chama cha Mameneja wa Ligi [LMA=League Managers Association] nini kilichotokea ili kuepusha kuonekana mbaya.

No comments:

Powered By Blogger