Thursday 29 October 2009

MAPACHA WA MAN U FABIO & RAFAEL WAMCHANGANYA REFA!!!!
Manchester United wamekata rufaa kwa FA kupinga Kadi ya Njano aliyopewa Fabio da Silva kwenye mechi ya Kombe la Carling hapo juzi walipowafunga Barnsley mabao 2-0 kwa madai kuwa Refa Chris Foy alijichanganya na kumpa Kadi wakati si yeye aliemchezea Rafu Winga wa Barnsley Jamal Campbell-Ryce.
Aliestahili kupata Kadi hiyo alikuwa ni Ndugu yake na Pacha mwenzake, Rafael, ambae wamefanana kupindukia.
Mapacha hao kutoka Brazil wamezaliwa Julai 9, 1990.
FA imethibitisha kupokea rufaa hiyo na itasikilizwa siku ya Jumanne na Kamisheni yao ya Sheria.
Katika mechi hiyo Manchester United walimaliza mechi wakiwa mtu 10 baada ya Nahodha wao Gary Neville kupewa moja kwa moja Kadi Nyekundu kwa kumvaa Adam Hammill ingawa ilionekana dhahiri Neville aliucheza mpira kwanza na ndipo akamgusa Mchezaji huyo wa Barnsley.
Kutolewa kwa Neville kulimfanya Sir Alex Ferguson atamke kuwa haishangazi kwa Nahodha wake kupewa Kadi Nyekundu kwa vile hali ya hewa ya sawa imeruhusu hayo.
Ferguson alikuwa akimaanisha jinsi wanavyominywa na Marefa katika mechi za hivi karibuni baada ya yeye kumponda Refa Alan Wiley na kumsema hayuko fiti.

No comments:

Powered By Blogger