Saturday 31 October 2009

LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii:
Leo ni dabi ya London Kaskazini: Arsenal v Tottenham!!!
*************************************************************
RATIBA LIGI KUU ENGLAND:
[Saa za Bongo]
Jumamosi, Oktoba 31
Arsenal v Tottenham [saa 9 dak 45 mchana]
[saa 12 jioni]
Bolton v Chelsea
Burnley v Hull
Everton v Aston Villa
Fulham v Liverpool
Portsmouth v Wigan
Stoke City v Wolverhampton Wanderers
Sunderland v West Ham
Manchester United v Blackburn Rovers [saa 2 na nusu usiku]
Jumapili, Novemba 1
[saa 1 usiku]
Birmingham v Manchester City
*******************************************************************************
Arsenal v Tottenham
Ligi Kuu England leo itaanza kuchezwa kwa pambano la Mahasimu wa Jiji moja, eneo moja, London Kaskazini, kati ya Arsenal na Tottenham Uwanjani Emirates.
Msimu uliokwisha, mechi kama hii, ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Harry Redknapp tangu ateuliwe Meneja wa Tottenham, mechi iliisha kwa suluhu ya 4-4.
Ushindani na ushabiki kwa pambano hilo tayari ushapamba moto huku Redknapp akisema Arsenal hawawezi kuchukua Ubingwa na akawapa Chelsea na Manchester United nafasi kubwa.
Juu ya yote, Tottenham haijawahi kuifunga Arsenal katika mechi yeyote ya Ligi kwa miaka 10 sasa.
Bolton v Chelsea
Vinara wa Ligi Kuu Chelsea leo wanasafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England kucheza na Bolton Wanderers na hii itakuwa mechi ya pili kati ya Timu hizi ndani ya wiki moja kwani majuzi kwenye Kombe la Carling Chelsea waliitandika Bolton 4-0 uwanjani Stamford Bridge.
Hata hivyo, Chelsea kati mechi 2 zilizopita za Ligi walizocheza ugenini zote wamefungwa na hilo pengine litawapa matumaini Bolton.
Fulham v Liverpool
Baada ya kuwafunga Mabingwa Manchester United bao 2-0 mechi iliyopita, leo Liverpool wapo Craven Cottage kucheza na Fulham bila Nahodha wao Steven Gerrard ambae bado ni majeruhi.
Kiungo mpya wa Liverpool, Alberto Aquilani, ambae alicheza robo saa katika kipigo cha Kombe la Carling Jumatano walichokipata kwa Arsenal, huenda leo akacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi.
Manchester United v Blackburn Rovers
Bila shaka leo Man U watashuka uwanjani huku wakitaka ushindi kwa kila hali baada ya kufungwa na Mahasimu wao Liverpool wiki iliyopita.
Man U leo huenda ikawa na pengo kwenye ulinzi kufuatia kuumia kwa Masentahafu Rio Ferdinand na Nemanja Vidic.
Blackburn nao wmekumbwa na gonjwa la Mafua ya Nguruwe hivyo inawezekana wakawakosa Wachezaji wao kama Chris Samba, Dunn na Jason Roberts.
Pengine kivutio kikuu kwenye mechi hii atakuwa Refa Phil Dowd ambae mechi yake ya mwisho kuichezesha Man U walipocheza na Fulham msimu uliopita aliwapa Kadi Nyekundu Scholes na Rooney na hivyo Wadau watafuatilia uchezeshaji wake hasa kufuatia ugomvi wa Sir Alex Ferguson na Marefa pale alipomsema Refa Alan Wiley hayuko fiti na baada ya hapo mechi zote za Man U zimekumbwa na maumuzi tata kwa Man U zikiwemo Kadi Nyekundu na kubeba wapinzani wao.

No comments:

Powered By Blogger