Wednesday 28 October 2009

Meneja wa Wigan adai Ferguson anaogopewa England!!!
Katika hali ya kushangaza na bila shaka ya kumuunga mkono Mhispania mwenzake Rafa Benitez, Meneja wa Wigan, Roberto Martinez, ameibuka na kudai Sir Alex Ferguson ana nguvu sana katika Soka la England na anaogopewa na FA, Chama cha Soka cha England.
Martinez pia amedai Ferguson anaungwa mkono na Mameneja wengi kuliko Benitez na ndio maana wanamuonea Benitez.
Bila shaka Martinez hajui kuwa kwa sasa Ferguson ameshitakiwa na FA kwa kauli yake kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti kauli aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu hapo Oktoba 3 kati ya Manchester United na Sunderland iliyomalizika 2-2 na kuibua mzozo mkubwa huku Chama cha Marefa wakitaka Ferguson apewe adhabu kali.
Wadau na Wachunguzi wa mambo wanahisi kauli ya Ferguson kumponda Refa Alan Wiley sasa imeanza kuisakama Manchester United kwani kwenye mechi Liverpool aliyoifunga Man U Jumapili bao 2-0 Refa Andre Marriner alionyesha waziwazi kuibeba Liverpool.
Martinez ametoa madai yake kwa kusema: “Ferguson yuko hapa ‘milele’ na ni mtu mzito! Ferguson ana kundi lake kama kina Steve Bruce aliekuwa Mchezaji wake na Sam Allardyce anaedhani atakuwa Meneja Man U Ferguson akiondoka!!”
Mechi ya pili mfululizo, Man U wapewa Kadi Nyekundu!!!
Katika mechi ya jana ya Kombe la Carling, Mabingwa Watetezi, Manchester United, waliifunga Barnsley bao 2-0 lakini walimaliza mechi wakiwa mtu 10 baada ya Nahodha wao Garry Neville kupewa Kadi Nyekundu licha ya kuonekana dhahiri akiucheza mpira kwanza na ndipo kumgusa Mchezaji wa Barnsley, Adam Hammill kwenye dakika ya 63.
Kitendo hicho kilimfanya Ferguson atamke: “Katika hali ya hewa ya sasa, Kadi hiyo Nyekundu inaeleweka!”
Mabao ya Man U yalifungwa na Danny Welbeck na Michael Owen.
Katika mechi zingine za Kombe la Carling hapo jana matokeo ni:
Blackburn 5 Peterborough 2
Portsmouth 4 Stoke 0
Sunderland 0 Aston Villa 0 [Aston Villa walishinda mechi hii kwa mikwaju ya penalti 3-1]
Tottenham 2 Everton 0
MECHI ZA LEO za KOMBE LA CARLING:
[saa 4 dak 45 usiku bongo taimu]
Arsenal v Liverpool
Chelsea v Bolton
Manchester City v Scunthorpe
Real Madrid yatandikwa na TIMU YA KIJIJINI!!!
Kwenye mechi ya Kombe la Mfalme wa Spain, Real Madrid imekung’utwa na Timu ya Kijijini inayocheza Daraja la 3, Alcorcon, kwa mabao 4-0 licha ya Real kuchezesha Kikosi chenye nguvu.
Kipigo hicho kimefanya zizagae habari kuwa endapo Real watafungwa mechi ya Ligi wikiendi ijayo watakapocheza na Getafe au kupigwa na AC Milan Jumanne ijayo kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, basi hiyo itakuwa baibai kwa Kocha Manuel Pellegrini.
Wachezaji wa Stoke City wapata dharura kwenye Ndege angani!!!
Ndege iliyokuwa imewabeba Wachezaji wa Stoke City wakiwa wanatoka kwenye mechi ya Kombe la Carling waliyofungwa na Portsmouth 4-0 ilipata hitilafu angani ikitokea Uwanja wa Ndege wa Southampton baada ya Wachezaji kumjulisha Rubani kuwa wanasikia harufu ya kuungua kitu na ikalazimu Ndege hiyo itue kwa dharura Uwanja wa Ndege wa Gatwick huku ikisindikizwa na Magari ya Faya.
Ingawa Ndege hiyo ilikaguliwa na kukutwa haikuwa na hitilafu, Timu ya Stoke City ilirudi nyumbani kwao kwa basi.
Portsmouth wapigwa marufuku kusajili Wachezaji!!
Klabu ya Portsmouth imezuiwa kusajili Wachezaji na Wasimamizi wa Ligi Kuu England hadi hapo watakapomaliza kulipa madeni ya Usajili na Ununuzi wa Wachezaji wanayodaiwa na Klabu nyingine.
Klabu hiyo ipo kwenye ukata licha ya kunuliwa na Tajiri kutoka UAE Sulaiman Al Fahim ambae baada ya kuimiliki wiki chache tu akamuuzia Mfanya Biashara wa Saudi Arabia Ali Al Faraj ambae amekiri hajui lolote kuhusu michezo na nia yake ilikuwa kuiuza kwa faida.
Wiki chache zilizopita Wachezaji wa Portsmouth walikosa mishahara na ikabidi Sulaiman Al Fahim atoe hela za dharura kuwalipa.

No comments:

Powered By Blogger