Saturday 31 October 2009

Mchezaji Marlon King alie lupango azua mjadala!!
Wenger asema akitoka jela aendelee kucheza!!
Mchezaji wa Wigan, Marlon King, aliefungwa miezi 18 kwa kumshambulia na kumvunja pua mwanamke ndani ya baa jijini London amezua mjadala mkali unaohusu ajira yake mara baada kutoka jela.
Mara baada ya hukumu hiyo, Klabu yake ya Wigan imesema itampa notisi ya siku 14 na kumfukuza.
Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan amezitaka Klabu za England zisimpe nafasi ya kucheza tena soka England.
Lakini Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amemtetea na kusema: “Naamini kuna sheria na haki hapa Uingereza na hiyo jela ndiyo haki aliyopata. Akimaliza kifungo yuko huru basi Klabu inayomtaka imchukue tu!”
Wachezaji wanne wa England wamo Listi ya FIFA ya Wagombea MCHEZAJI BORA DUNIANI!!!
Ni Terry, Lampard, Gerrard na Rooney!!
Mastaa wa England John Terry, Frank Lampard, Steven Gerrard na Wayne Rooney ni miongoni mwa Listi ya Wachezaji 23 watakaoshindania Tuzo ya MCHEZAJI BORA DUNIANI WA MWAKA.
Miongoni mwao yumo Lionel Messi anaetegemewa kuinyakua Tuzo hiyo na pia yumo Mshindi wa mwaka jana Cristiano Ronaldo.
Kwa upande wa Wanawake kuna majina 10 likiwemo la Marta wa Brazil Mshindi wa mwaka jana.
Manahodha na Makocha wa Timu za Taifa ndio watawapigia kura wagombea na Washindi wa 5 wa juu watakaoingia fainali watatangazwa mwanzoni mwa Desemba.
Mshindi wa Tuzo atatangazwa Desemba 21.
Listi kamili:
WANAUME: Michael Ballack, Gianluigi Buffon, Iker Casillas, Cristiano Ronaldo, Diego, Didier Drogba, Michael Essien, Samuel Eto’o, Steven Gerrard, Thierry Henry, Zlatan Ibrahimovic, Andres Iniesta, Kaka, Frank Lampard, Luis Fabiano, Lionel Messi, Carles Puyol, Franck Ribery, Wayne Rooney, John Terry, Fernando Torres, David Villa, Xavi.
WANAWAKE: Nadine Angerer, Sonia Bompastor, Cristiane, Inka Grings, Mana Iwabuchi, Simone Laudehr, Marta, Brigit Prinz, Kelly Smith, Abby Wambach.

No comments:

Powered By Blogger