Sunday 11 January 2009

FA kuchnguza kauli za Benitez za kumshambulia Ferguson, Wenger ammshangaa Benitez!!

Chama cha Soka cha England, FA, kimetoa tamko kwamba wanazichunguza kauli kali za Meneja wa Liverpool zilizomshambulia Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson na kumtuhumu anaua Marefa na huwa hachukuliwi hatua yeyote na FA.
FA imesema itatoa tamko lake wiki ijayo.
Mpaka sasa Sir Alex Ferguson hajazungumza chochte kuhusu matamshi ya Benitez.
Nae Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema amestushwa na kauli za Benitez: 'Inashangaza lakini sidhani kauli hizi zinamtisha Ferguson ila nadhani uhusiano kati ya Benitez na Ferguson utaathirika.'


WACHEZAJI BORA WA 2008 WA FIFA KUTANGAZWA KESHO!!!

Kesho ndani ya Jumba la Zurich Opera huko Uswisi dunia itatambulishwa kwa Wachezaji wawili Bora wa Dunia kwa mwaka 2008, mmoja akiwa kutoka kwa Wanaume na mwingine ni upande wa Wanawake.
Kaka, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Fernando Torres na Xavi ni Wagombea kwa upande wa Madume na Nadine Angerer, Cristiane, Marta, Birgit Prinz na Kelly Smith ni toka kundi la Wanawake.
Wanaopewa nafasi kubwa kushinda ni Cristiano Ronaldo na Marta, Mwanamke hodari sana toka Brazil ambae pia alikuwa Mshindi kwa Mwaka 2007.
Marta anaonekana pichani kulia akiwa na Mshindi wa Wanaume wa Mwaka 2007 Kaka wa AC Milan na Brazil.


No comments:

Powered By Blogger