Monday 1 June 2009

ANCELOTTI BOSI MPYA CHELSEA!!!
Klabu ya Chelsea imemwajiri Mtaliana Carlo Ancelotti [49] kuwa Meneja mpya wa Klabu hiyo na amepewa mkataba wa miaka mitatu.
Jana Ancelotti aliiwezesha Klabu yake AC Milan kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi ya Serie A huko Italia na hivyo kuweza kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao na mara baada ya mechi ya jana kumalizika akatangaza kuachia ngazi AC Milan.
Ancelotti sasa ni Meneja wa 5 hapo Chelsea katika kipindi cha miezi 21 iliyopita na waliomtangulia ni Claudio Ranieri, Jose Mourinho, Avram Grant, Luis Filipe Scolari na Guus Hiddink.
Carlo Ancelotti ataanza rasmi kazi yake Julai 1.

UEFA yatangaza majaribio ya Waamuzi Watano kwenye mechi!!!

UEFA, Chama cha Soka cha Ulaya, kimetangaza kuwa msimu ujao kwenye Mashindano mapya ya UEFA EUROPA LEAGUE ambayo yalikuwa yakiitwa UEFA CUP majaribio ya kuwa na Waamuzi watano kwenye mechi moja yatafanyika.
Mbali ya Refa na Wasaidizi wake wawili Washika Vibendera wanaokaa pembeni mwa Uwanja kutakuwa na Wasaidizi wengine wawili wa ziada watakaokaa nyuma ya goli kila mmoja.
Waamuzi hawa watano watakuwa wakiwasiliana kwa kutumia redio.
Majaribio ya Waamuzi watano yalifanyika kwenye mechi za Nchi za Ulaya ya Vijana wa chini ya miaka 19 yaliyozikutanisha Nchi za Slovenia, Cyprus na Hungary na UEFA kuridhika na mafanikio yake na sasa wanataka kuyapeleka ngazi ya juu zaidi.

No comments:

Powered By Blogger