Wednesday 3 June 2009

Birmingham yamchukua Benitez
Timu mpya kwenye LIGI KUU England msimu ujao Birmingham City imevunja rekodi yao ya dau la uhamisho kwa kumsajili Mshambuliaji kutoka Ecuador Christian Benitez kutoka Klabu ya Mexico Santos Laguna.
Ingawa ada ya uhamisho haikutajwa lakini inaaminika ni zaidi ya Pauni Milioni 6.25 Klabu hiyo ililipa kumchukua Emile Heskey mwaka 2004 na hizo zikiwa ni fedha nyingi sana kwa wao kulipa kwa Mchezaji yeyote.
Benitez, 23, alifunga magoli 31 katika mechi za Ligi huko Mexico na ni Mtoto wa aliewahi kuwa Mfungaji Bora wa Nchi ya Ecuador, Ermen Benitez.
Christian Benitez alicheza Kombe la Dunia akiwakilisha Ecuador mwaka 2006 huko Ujerumani.

Nani aupinga uvumi kuwa Man U watambwaga!!!
Winga kutoka Ureno, Nani, anaechezea Manchester United amepuuza uvumi uliotapakaa kuwa Klabu yake inafikiria kumuuza kabla msimu mpya haujaanza.
Nani alijiunga kutoka Sporting Lisbon mwaka 2007 kwa ada ya Pauni Milioni 17 lakini hana namba ya kudumu Kikosini mwa Man U na mwenyewe amezipinga tetesi hizo kwa kutamka: ‘Maisha yangu ya baadae ni Man U! Nimetwaa Mataji mawili sasa na ni fahari kubwa kuwa na Klabu kubwa kama hii! Siondoki na wala siendi kokote kwa mkopo! Ntamaliza mkataba wangu hapa!’
MDHAMINI MPYA KWENYE JEZI ZA MAN U ATOA DAU LITAKALOWEKA REKODI YA DUNIA !!!
Manchester United wamepata Mdhamini mpya badala ya AIG, Kampuni ya Bima ya Kimarekani iliyodhoofika mno kutokana na mporomoko wa soko la dunia, ambayo jina lake lipo kifuani mwa jezi za Man U.
Mkataba wa Man U na AIG utamalizika Juni 2010 na AIG ilishatamka mapema hawatuongeza tena mkataba kwa sababu hali yao ni mbaya kiuchumi. AIG walikuwa wakiilipa Man U Pauni Milioni 14 kwa mwaka kwa kuweka jina la AIG kifuani mwa jezi.
Sasa Manchester United wamekubaliani na Kampuni kubwa ya huko Chicago, Marekani iitwayo Aon inayoshughulika na Mambo ya Fedha na Aon watawalipa Man U Pauni Milioni 20 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka minne na hili ni dau kubwa kabisa kwa Klabu yeyote duniani kulipwa na Mdhamini.
Wadhamini wakubwa wanaozilipa Klabu kubwa duniani kwa majina yao kuonekana kwenye jezi ni:
-Bayern Munich - £17 Milioni kwa mwaka na T-Home, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu.
-Real Madrid - £15 Milioni kwa mwaka na Kampuni ya Austria ya Kamari Bwin.com.
-Juventus - £15m kwa mwaka na Kampuni ya Libya ya mafuta Tamoil.
-Chelsea - £10 kwa mwaka na Kampuni ya Elektroniki ya Korea Samsung.
-Liverpool - £8m kwa mwaka na Kampuni ya Bia Carlsberg.
-Manchester City - £8 kwa mwaka na Kampuni ya Ndege ya huko Falme ya Nchi za Kiarabu Etihad Airways.

No comments:

Powered By Blogger