Wednesday 3 June 2009

Steve Bruce athibitishwa Bosi mpya Sunderland!!!!

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Steve Bruce [48], amethibitishwa na Klabu ya Sunderland kuwa ndie Meneja mpya na amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Steve Bruce anachukua nafasi ya Ricky Sbragia alieachia ngazi siku ya mwisho ya msimu wa LIGI KUU England mara tu baada ya Sunderland kupuruchuka kushushwa Daraja.
Sbragia alirithi cheo hicho toka kwa Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane aliebwaga manyanga mwenyewe Desemba mwaka jana.
Steve Bruce ameshawahi kuwa Meneja kwenye Klabu za Sheffield United, Huddersfiled, Crystal Palace, Birmingham na Wigan alikokuweko kwa vipindi viwili tofauti na ndiko alikotokea na kuhamia Sunderland.
Owen Hargreaves huenda asiendelee kucheza?
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa na Klabu ya Manchester United lakini zinapamba moto kwenye Vyombo vya Habari kuwa Owen Hargreaves [28] wa Manchester United ambae alifanyiwa operesheni mbili kwenye kila goti lake huenda asirudi tena uwanjani na nyingine zinadai hata akirudi basi hawezi kucheza kwa muda mrefu.
Owen Hargreaves alisajiliwa kutoka Klabu kongwe ya Ujerumani Bayern Munich Julai 2007 kwa dau la Pauni Milioni 17 na amemudu kuanza mechi 25 tu hapo Man U.
Hargreaves mara ya mwisho aliichezea Man U Septemba 21, 2008 ilipotoka sare 1-1 na Chelsea huko Stamford Bridge kwenye mechi ya LIGI KUU na mwezi Novemba akapelekwa Marekani kufanyiwa operesheni ya goti lake la kulia kwa Mpasuaji stadi Daktari Richard Steadman na Januari akafanyiwa tena operesheni goti jingine la kushoto.
Daktari Steadman ameshawapasua kwa mafanikio makubwa sana Mastaa mbalimbali duniani akiwemo Mcheza Gofu maarufu Tiger Woods, Wanasoka Michael Owen, Alan Shearer na Ruud van Nistelrooy.
Tarehe 27 Mei 2009 kabla ya kuanza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Roma, Italia kati ya Manchester United na Barcelona, Owen Hargreaves alionekana akipiga danadana mpira huku Wachezaji wa Man U wakipasha moto.

No comments:

Powered By Blogger