Tuesday 2 June 2009

Perez kuapishwa Rais wa Real Madrid leo, Pellegrini ateuliwa Kocha!
Florentino Perez leo ataapishwa kama Rais mpya wa Klabu ya Spain Real Madrid na sasa dunia isubiri tu ngonjera za kuchukuliwa Christiano Ronaldo, Cesc Fabregas, Xavi Alonso na Mastaa kadhaa kwenda huko Spain.
Florentino Perez, miaka 62, ni tajiri mwenye shughuli za Ujenzi, na aliwahi kuwa Rais wa Real kati ya mwaka 2000 na 2006 na katika kipindi hicho aliweza kuwasajili Zinedine Zidane, Ronaldo, Luis Figo and David Beckham. Vilevile, alimudu kutwaa La Liga mara 2, UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara moja na Real kubatizwa jina la ‘Galacticos!’
Mara tu baada ya kutangazwa Perez Rais, Real Madrid ikatoa tamko rasmi kuwa aliekuwa Bosi wa Villareal Manuel Pellegrini [pichani], anaetoka Chile, ndie Kocha mpya.
Pellegrini, 55, atakuwa Meneja wa 8 kwa Real Madrid katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Fabregas ataka Alonso asainiwe Arsenal!!
Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, ameitaka Klabu yake Arsenal imsajili Kiungo wa Liverpool Xabi Alonso ambaye ni Mhispania mwenzake.
Fabregas amesema: ‘Tumepoteza Wachezaji wakubwa na Meneja anajua hilo. Lakini tunaweza kusaini Wachezaji wakubwa! Tunahitaji mtu kwenye Kiungo atakaeleta ushindani na kutupa mwelekeo mwingine! Alonso ni bora na anafunga magoli!’

No comments:

Powered By Blogger