Tuesday, 2 June 2009

Blackburn Rovers wamsaini Mchezaji kutoka Bondeni!!!!!
Elrio van Heerden, Mchezaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini, anaechezea Klabu ya Ubelgiji ya Club Brugge ambako alikaa kwa miaka mitatu amesaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Blackburn Rovers inayocheza LIGI KUU England.
Heerden, 25, alikuwa kambini na Timu ya Afrika Kusini inayojitayarisha kwa Kombe la Mabara lakini akaruhusiwa kwenda England kusaini mkataba na huyu ndie Mchezaji wa kwanza kwa Meneja wa Blackburn Rovers Sam Allardyce kumsajili majira haya ya joto ambako Timu za LIGI KUU zinasubiri msimu kuanza upya mwezi wa Agosti.
Heerden atajumuika na Mchezaji mwingine kutoka Afrika Kusini, Benni McCarthy, hapo Ewood Park lakini Mchezaji mwingine wa Afrika Kusini aliekuwepo hapo Blackburn Rovers Aaaron Mokoena amehama hivi karibuni kwenda Portsmouth
Nahodha wa Villa Barry afanya mazungumzo na Man City!!
Kiungo na Nahodha wa Aston Villa, Gareth Barry, amepewa baraka na Klabu yake kuongea na Manchester City ili kufikia muafaka ahamie Man City.
Barry, 28, msimu uliokwisha alibakia kidogo kuhamia Liverpool lakini kukawa na mvutano kuhusu dau la uhamisho na dili ikavunjika.
Ingawa Villa imefanikiwa kuingia na kucheza Ulaya msimu ujao ambako watacheza kwenye Mashindano mapya yatakayojulikana kama UEFA EUROPA LEAGUE na Man City hawachezi Ulaya kwa kumaliza nafasi duni kwenye LIGI KUU, inaaminika mvuto pekee unaomfanya Barry kuhama Villa Klabu aliyoichezea tangu 1997 ni dau kubwa huko Man City.
Barry, ambae ameichezea Villa jumla ya mechi 443, kwa sasa yuko kambini na Timu ya Taifa ya England inayojitayarisha kwa mechi za mchujo wa kuwania kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 watakapocheza na Kazakhstan Jumamosi na Andorra siku nne baadae.

No comments:

Powered By Blogger