Tuesday 2 June 2009

RIO NJE ENGLAND!!!
Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand, ametolewa kwenye Kikosi cha England kinachokwenda kucheza na Kazakhstan siku ya Jumamosi katika mechi ya mchujo wa kugombea kuingia Fainali Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini baada ya kusumbuliwa na misuli ya mguu.
Nafasi yake amepewa Beki wa Bolton, Gary Cahill, ambae huchezea Timu ya Taifa ya England ya Vijana wa chini ya miaka 21.
Hata hivyo, habari toka kambini kwa England zimesema Rio Ferdinand kama atapata afueni huenda akacheza mechi ijayo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Jumatano ijayo na Andorra Uwanjani Wembley, London.

Huyu ni Mchezaji wa pili wa Manchester United kutoka kwenye Kikosi cha England baada ya Michael Carrick ambae nae ni majeruhi.
Haya kumekucha........mara baada ya kuukwaa Uraisi Real, Perez kishawavamia Alonso na Ronaldo!!!!
Kama ilivyotabiriwa na hata haijapita hata siku moja, Rais mpya wa Real Madrid, Florentino Perez, ameshaanza kubwabwaja na kudai Cristiano Ronaldo wa Manchester United na Xabi Alonso wa Liverpool [pichani]wanawavutia sana na ni Wachezaji wanaofaa Real Madrid.
Ingawa Perez hajatamka na kuweka bayana kama Real Madrid watatoa ofa rasmi kwa Klabu husika za Ronaldo na Alonso lakini kauli zake zinadokeza nia wanayo.
Perez alitamka: ‘Kuna dili nyingine zinachukua siku chache, nyingine miezi! Lakini tuna muda hadi Agosti 31.’
Agosti 31 ndio siku ya mwisho dirisha la uhamisho Wachezaji kufungwa.

No comments:

Powered By Blogger