Tuesday 2 June 2009

NI RASMI: MAN CITY WAMCHUKUA NAHODHA WA VILLA BARRY!!!
Manchester City wamemnunua Kiungo na Nahodha wa Aston Villa, Gareth Barry [28], kwa kitita cha Pauni Milioni 12 na amesaini mkataba wa miaka mitano.
Barry, ambae amechezea England mechi 29, msimu uliokwisha alibakia kidogo tu kuhamia Liverpool lakini kukawa na mvutano kuhusu dau la uhamisho na dili ikavunjika.
Wamiliki wa Manchester City, Abu Dhabi United Group, mali ya Koo ya Kifalme ya Abu Dhabi ambao ni sehemu ya Nchi Tajiri sana ya Falme ya Nchi za Kiarabu, inaaminika watamwaga ‘vijisenti’ kipindi hiki ili kupata Wachezaji wengi ili kuimarisha Timu yao. Barry, ameichezea Villa jumla ya mechi 443 tangu mwaka 1997, kwa sasa yuko kambini na Timu ya Taifa ya England inayojitayarisha kwa mechi za mchujo wa kuwania kucheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 watakapocheza na Kazakhstan Jumamosi na Andorra siku nne baadae

No comments:

Powered By Blogger