Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameomba msamaha kwa Refa Alan Wiley kwa kauli yake kwamba Refa huyo hayuko ‘fiti’ kuchezesha mechi kauli aliyoitoa mara baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Manchester United na Sunderland iliyoisha 2-2 huko Old Trafford wikiendi iliyokwisha.
Mara baada ya kauli hiyo ya Sir Alex Ferguson, FA, Chama cha Soka England, kilimwandikia barua Ferguson kumtaka ajieleze. Taarifa iliyotoka kwenye tovuti ya Manchester United imemkariri Ferguson akisema: “Naomba msamaha kwa Bw. Wiley kwa kumfedhehesha na kwa FA kwa kutoa mawazo yangu hadharani. Haikuwa nia yangu kumfanya Bw. Wiley amulikwe na Waandishi wa Habari. Nia yangu ni kukutana nae na kumwomba msamaha uso kwa uso mara nitakaporudi safari yangu nje ya Nchi.”
Ferguson aliongeza kwamba anamheshimu Refa Wiley na kauli yake haikumaanisha:
-Wiley ni Refa mbaya.
-Wiley anapendelea.
-Uamuzi wake kwenye mechi ile ulikuwa dhaifu.
-Kwamba alipitwa na matukio muhimu kwenye mechi ile.
Mara baada ya Ferguson kusema maneno kwamba Wiley ‘hayuko fiti’ mjadala na mzozo mkubwa uliibuka kwenye Vyombo vya Habari huko England.
No comments:
Post a Comment