Wednesday 7 October 2009

Grant arudi Portsmouth!!
Aliekuwa Kocha wa Chelsea, Avram Grant, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Soka wa Portsmouth na atakuwa akishirikiana na Meneja Paul Hart kuinasua Klabu hiyo iliyo mkiani Ligi Kuu England.
Grant aliwahi kuwa Portsmouth mwaka 2006 kama Mkurugenzi wa Soka wakati huo Meneja akiwa ni Harry Redknapp lakini alihamia Chelsea Septemba 2007 Jose Mourinho alipoondoka Chelsea.
Grant aliifikisha Chelsea Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka jana mwezi Mei na ikatolewa na Manchester United kwa penalti na baada ya mechi hiyo akatimuliwa Chelsea.
Mahakama Uswisi yasimamisha ulipaji Fidia wa Mutu kwa Chelsea
Mahakama huko Uswisi imesimamisha kwa muda kulipwa kwa Fidia aliyotakiwa Adrian Mutu kuilipa Chelsea na FIFA baada ya kufungiwa alipokutwa na chembechembe za Kokeni na kisha kufukuzwa Chelsea.
Mutu aliamriwa na FIFA kulipa Pauni Milioni 15 na adhabu hiyo iliungwa mkono na Mahakama ya Usuluhishi Michezoni [CAS ambako Mutu alikata rufaa.
Wakala wa Mutu, Victor Becali, amethibitisha uamuzi wa Mahakami hiyo wa kusimamisha ulipwaji fidia hadi Novemba ili isikilize Kesi ya Mutu.
Mutu mwenyewe amesema hana pesa za kulipa fidia hiyo.

No comments:

Powered By Blogger