Wednesday, 7 October 2009

Wenyeji Misri nje Kombe la Dunia!!!
Wenyeji Misri jana wamebwagwa nje ya Kombe la Dunia la Vijana wa Chini ya Miaka 20 baada ya kufungwa 2-0 na Costa Rica ambao sasa wameingia Robo Fainali na watacheza na Mshindi kati ya UAE na Venezuela wanaokutana leo.
Ghana nao wamesonga mbele na kuingia Robo fainali baada ya kuifunga South Africa 2-1 katika muda wa nyongeza baada ya mechi kwisha dakika 90 mabao yakiwa 1-1.
Hungary na Czech Republic zilitoka suluhu 2-2 hadi muda wa nyongeza na penalti tano tano zikawapa ushindi wa penalti 4-3.
MECHI ZA LEO Jumatano, Oktoba 7:
Brazil v Uruguay
Venezuela v UAE
Germany v Nigeria
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea v Ghana
09/10/09: Italy v Hungary
10/10/09: Brazil AU Uruguay v Germany AU Nigeria
10/10/09: Venezuela AU UAE v Costa Rica
Van der Sar arudi golini baada ya kuumia 
Kipa wa Manchester United Edwin van der Sar jana alimaliza dakika 90 za mechi ya Vikosi vya Akiba kati ya Manchester United na Everton ambayo Man U walishinda kwa bao 1-0 mfungaji akiwa Federico Macheda.
Kipa huyo Mdachi mwenye umri wa miaka 38 hajaonekana Uwanjani tangu Agosti 5 alipocheza mechi ya kugombea Kombe la Audi huko Ujerumani na Bayern Munich na kuvunjika mifupa miwili ya mkono wa kushoto.
Kutokuwepo kwa Van der Sar kulimpa nafasi Kipa Ben Foster kucheza lakini Kipa huyo wa akiba ameonekana kupwaya sana na amekuwa akitoa zawadi ya magoli.
Foster alikuwa lawamani kwa goli lililofungwa na Gareth Barry katika mechi na Manchester City na pia siku ya mechi ya Sunderland bao la pili la Mshambuliaji Kenwyne Jones linasemwa kuwa ni kosa lake.
Foster hakuchaguliwa kwenye Timu ya Taifa ya England itayocheza mechi za Kombe la Dunia Jumamosi hii na Jumatano ijayo dhidi ya Ukraine na Belarus ingawa kuachwa kwake kunasemekana ni kuugua kifua.
Van der Sar anatarajiwa kurudi golini kwenye mechi ya Ligi Kuu tarehe 17 Oktoba Man U watakapokwaana na Bolton.

No comments:

Powered By Blogger