Saturday 10 October 2009

Rio asema akiachwa Fainali Kombe la Dunia akiwa sio fiti halalamiki!!
Rio Ferdinand amesema akiikosa Fainali ya Kombe la Dunia mwakani kwa sababu hayuko fiti au ni majeruhi hawezi kulalamika kwa sababu Meneja wa sasa hajali majina bali huchagua Wachezaji fiti tu na walio kwenye fomu tu.
Rio amezungumzia hilo hasa kwa vile yeye kwa sasa anasakamwa na majeruhi mfululizo yaliyomfanya katika mwaka huu acheze mechi 26 kati ya 40 angezoweza kuchezea Klabu yake Manchester United na England.
Rio, atakaetimiza miaka 30 mwezi ujao, amesema: “Capello ni mkweli! Ameweka bayana anachagua mtu akiwa fiti na kwenye fomu tu na sio jina! Maishani sijaandamwa na majeruhi kama sasa! Na si tatizo moja tu linalonisumbua! Msimu uliokwisha niliumia mgongo, msimu huu nimeumia musuli nyuma ya ugoko na kisha musuli pajani! Ni vitu tofauti na sasa nafanyiwa mazoezi ili kujifua nisipate matatizo ya aina hii!”
Rio Ferdinand anategemewa kucheza mechi ya leo ya Kombe la Dunia ugenini na Ukraine.
Rooney na Ronaldo wataniana!!
Fowadi wa England, Wayne Rooney, ambae Timu yake ishafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani huku wakiwa wamebakisha mechi mbili amesema atafurahi sana ikiwa Cristiano Ronaldo na Ureno yake watashindwa kwenda Fainali hizo.
Ureno iko hatarini kuzikosa Fainali hizo na wako nafasi ya 3 Kundini mwao pointi 2 nyuma ya Sweden walio nafasi ya pili huku Denmark akiongoza Kundi hilo.
Rooney alisema: “Katika Kombe la Dunia mwaka 2006 Ureno walitung’oa Robo Fainali na mie nilipewa Kadi Nyekundu! Na tulipotolewa EURO 2008 Ronaldo alitucheka sana tulipokuwa nae Manchester United! Sasa bora wao wasiende Afrika Kusini!”
Ronaldo alipoulizwa kuhusu kauli ya Rooney alijibu kuwa anadhani rafiki yake huyo anawatania tu.

No comments:

Powered By Blogger