Tuesday, 6 October 2009

Refa Mstaafu amponda Fergie!!!
Fergie atakiwa na FA kujieleza!!
Jeff Winter ambae amestaafu baada ya kuwa mmoja wa Marefa wa Ligi Kuu England amemponda Sir Alex Ferguson kwa kauli yake aliyoitoa mara baada ya dro ya 2-2 ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester United na Sunderland alipomsema Refa aliechezesha mechi hiyo Alan Wiley kuwa hayuko ‘fiti’.
Jeff Winter amesema kauli za Ferguson ni za uburuzaji na kiwoga na pia amedai Ferguson alitoa kauli hizo ili kuficha ukweli kuwa Timu yake Man U ilicheza vibaya mechi hiyo.
Winter amesema: “Nadhani safari hii Ferguson amezidisha na hili linaweza kuwaathiri Manchester United na huenda Marefa wakaungana na kuikomoa Timu hiyo kwenye mechi zao!”
Klabu ya Manchester United imekataa kuzungumza lolote kuhusu kauli za Refa huyo wa zamani.
Wakati huohuo, FA imemtaka Sir Alex Ferguson atoe ufafanuzi kuhusu kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fiti
Mmiliki wa Portsmouth auza hisa zake wiki 6 tu baada ya kuzinunua!!
Sulaiman al-Fahim, ambae aliinunua Portsmouth wiki 6 zilizopita, ameamua kuuza aslimia 90 ya hisa hizo kwa Tajiri kutoka Saudi Arabia Ali al-Faraj.
Uamuzi huo umekuja huku Klabu ya Portsmouth ikishindwa kuwalipa Wachezaji wake mishahara.
Sulaiman al-Fahim ndie alishiriki kuinunua Klabu ya Manchester City kwa ajili ya Koo mojawapo ya Kifalme ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.
Mmiliki wa Liverpool George Gillett amlaumu Rafael Benítez kwa matokeo mabaya!!!
George Gillett, mmoja wa Wamarekani wawili ambao ndio Wamiliki wa Liverpool amedai Rafael Benitez ndie alaumiwe kwa matokeo mabaya ya Liverpool ambao juzi walifungwa na Chelsea mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu. Gillett amedai yeye na Mmiliki mwenzake Tom Hicks wametoa dau la kutosha kuifanya Liverpool ipate Wachezaji bora na kuhakikisha mafanikio lakini kama hilo linaonekana haliwezekani basi wa kulaumiwa ni Benitez.
Gillettte amesema: “Sisi tumewekeza pesa nyingi kupita hata Klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United!”
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Spain na Paraguay zatinga Robo Fainali.
Jana Italia na South Korea zimekuwa Timu za kwanza kuingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 20 baada ya kuzichabanga Timu zilizopewa nafasi kubwa kufanya vizuri Spain na Paraguay.
Spain ilipigwa 3-1 na Italy na South Korea iliikung’uta Paraguay 3-0.
Raundi ya Pili inaendelea leo kwa mechi zifuatavywo:
MECHI ZA LEO Jumanne, Oktoba 6:
Ghana v South Africa
Egypt v Costa Rica
Hungary v Czech Republic

No comments:

Powered By Blogger