Sunday 4 October 2009

ZE BIGI MECHI: Chelsea 2 Liverpool 0
Hadi mapumziko mechi ilikuwa ngumu na suluhu lakini ushirikiano mwema kati ya Washambuliaji hatari wa Chelsea Didier Drogba aliempa pande tamu Nicolas Anelka dakika ya 59 na kupachika bao la kwanza ndio uliwafungulia njia Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge na kuwanyuka Liverpool 2-0 na kuchukua uongozi wa Ligi Kuu England.
Alikuwa tena Didier Drogba aliefanya kazi ya punda kwa kupigana na Mabeki wawili wa Liverpool katika dakika ya 91 na kuingia nao mpira ndani ya boksi na kuupenyeza kumfanya Malouda afunge bao la pili.
Chelsea wako kileleni wakiwa na pointi 21 na Mabingwa Watetezi Manchester United ni wa pili wakiwa na pointi 19.
West Ham 2 Fulham 2
Goli la dakika za majeruhi la Junior Stanislas limewapa West Ham suluhu ya bao 2-2 dhidi ya mtu 10 Fulham na kuwafanya wapate pointi ya kwanza Uwanja wa nyumbani Upton Park tangu ligi ianze.
Carlton Cole aliwapa uongozi West Ham dakika ya 16 na pengine walitegemea ubwete hasa baada ya Fulham kupata pigo kwa Mchezaji wao kutoka Afrika Kusini aliekuwa akicheza mechi yake ya kwanza, Kagisho Dikgacoi, kupewa Kadi Nyekundu na Refa Phil Dowd baada ya kuvaana na Scott Parker wa West Ham huku mpira ukiwa haupo kwao.
Refa Phil Dowd aliwapa Dikgacoi na Parker Kadi za Njano lakini ghafla akabadili uamuzi baada ya kuwasiliana na Msaidizi wake na kumpa Nyekundu Dikgacoi.
Kipindi cha pili Fulham walisawazisha dakika ya 47 kwa penalti iliyopigwa na Danny Murphy na kuongeza bao kupitia Gera dakika ya 57.
Everton 1 Stoke City 1
Robert Huth aliwapa uongozi Stoke daki ya 50 kufuatia kona lakini Leon Osman alisawazisha kwa Everton dakika ya 55 kwa bomba murua.

No comments:

Powered By Blogger