Thursday, 8 October 2009

LISTI YA MAMENEJA MATAJIRI ENGLAND YATAJWA!!
Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Timu inayosuasua mkiani Daraja la Coca Cola Championship, Ipswich Town, anashikilia nafasi ya pili katika Listi ya Mameneja Matajiri huko England.
Roy Keane amethaminiwa kuwa na utajiri wa Pauni Milioni 27.
Anaeshika nambari wani ni Fabio Capello mwenye Pauni Milioni 30.
Sir Alex Ferguson wa Manchester United ni wa tatu akiwa na Pauni Milioni 22.
Listi ya Mameneja Matajiri 10 ni:
-Fabio Capello [England] Pauni Milioni 30
-Roy Keane [Ipswich] Pauni Milioni 27
-Sir Alex Ferguson [Manchester United] Pauni Milioni 22
-Carlo Ancelotti [Chelsea] 17
-Sven-Goran Eriksson [Notts County]
-Arsene Wenger [Arsenal] 15
-Harry Redknapp [Tottenham] 10
-Rafael Benitez [Liverpool] 9
-Martin O’Nell [Aston Villa] 9
-Mark Hughes [Man City] 8
FIFA yairuhusu Man U kumsajili Kinda Pogba!!!
Manchester United imeruhusiwa na FIFA kumsajili Kijana mdogo wa miaka 16 Paul Pogba baada ya Klabu ya Ufaransa Le Havre awali kuweka pingamizi kuwa Man U imempora Mchezaji huyo.
Mwezi Septemba Chelsea ilifungiwa na FIFA kwa kumrubuni na kumsaini kinyume cha sheria Gael Kakuta mwaka 2007 na hivyo kupewa adhabu ya kutosajili Mchezaji yeyote hadi 2011.
Lakini Jaji aliyeteuliwa na FIFA kuipitia kesi ya Le Havre na Manchester United kuhusu Paul Pogba aliamua kuwa kwa sababu Pogba ni mdogo haiwezekani kisheria Le Havre wawe na mkataba na Pogba kuichezea Klabu hiyo ya Ufaransa kama Mchezaji wa Kulipwa.
Uamuzi huo wa FIFA umewaruhusu Manchester United kumsajili Pogba kwenye Chuo chao cha Soka.
Mwezi uliokwisha Manchester United iliwatishia kuwashitaki Le Havre kwa kuwachafulia jina lao kwa madai kuwa wamemwiba Pogba.
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Brazil, UAE na Germany zajikita Robo Fainali!!
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumatano, Oktoba 7:
Brazil 3 v Uruguay 1
Venezuela 1 v UAE 2
Germany 3 v Nigeria 2
ROBO FAINALI:
09/10/09: South Korea v Ghana
09/10/09: Italy v Hungary
10/10/09: Brazil v Germany
10/10/09: UAE v Costa Rica

No comments:

Powered By Blogger