Sunday 4 October 2009

Steve Bruce ajutia kuibwaga nafasi kuwafunga Man U!!
Bosi wa Sunderland aliewahi kuwa Nahodha wa Manchester United, Steve Bruce, amesikitishwa na Timu yake kuipoteza nafasi ya kuifunga Manchester United Old Trafford pale walipojifunga wenyewe dakika za majeruhi na kufanya mechi hiyo iishe 2-2.
Beki wa Sunderland, Anton Ferdinand, mdogo wake Rio Ferdinand wa Man U, aliukwamisha mpira wavuni katika harakati za kuokoa katika dakika ya 92 na kuipa Man U dro ya 2-2.
Katika mechi hiyo ya jana, Sunderland waliongoza mara mbili kwa magoli ya Darren Bent na Kenwyne Jones lakini Man U walisawazisha.
“Inasikitisha!” Bruce alisema. “Sizijui takwimu zinasemaje lakini hii ni kawaida ya Man U kusawazisha au kushinda dakika za majeruhi! Hata kama hawachezi vizuri, huwa wanapata matokeo mazuri! Nadhani Ayatollah mwenyewe hukaa na kuwatazama!”
Beckham kurudi tena San Siro Januari
David Beckham amefichua kwamba yuko mbioni kukamilisha makubaliano ya yeye kurudi kuichezea tena AC Milan mwezi Januari mwakani wakati msimu wa Soka huko Marekani utakaposimama ili kuweka hai mategemeo yake ya kuichezea England kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Kocha wa England Fabio Capello ameshatamka kuwa ni lazima Beckham arudi kucheza Ulaya ili achaguliwe England.
Msimu uliokwisha Beckham aliichezea AC Milan kwa mkopo na hilo lilimwezesha kuendelea kuichezea England.
Ingawa kuna Klabu nyingi zinamtaka, akiwamo Harry Redknapp wa Tottenham, Beckham mwenyewe amesema hawezi kurudi kucheza England.
Beckham anatamka: “Siku zote nimesema, baada ya kuondoka Man United siwezi kurudi England kuchezea Klabu nyingine! Hiyo ni ngumu kwangu!”
Kwa sasa Beckham anachezea LA Galaxy kwenye Ligi ya Marekani ijulikanayo kama MLS .
Roy Keane awa mbogo kwa Maripota!!!
Meneja wa Ipswich, ambae alikuwa Nahodha wa Manchester United, Roy Keane, ambae Timu yake ipo mkiani kwenye Ligi ya Coca Cola Championship, amewafokea Waandishi mara baada ya mechi ambayo Ipswich ilifungwa 2-1 na Barsnley hapo jana.
Alipohojiwa na Mwandishi mmoja kama atabaki kuendelea kuwa Meneja baada ya Timu yake kutoshinda hata mchezo mmoja katika 10 waliyocheza tangu Ligi ianze, Keane alijibu: “Sitaki kujibu swali hilo”
Alipoendelea kuulizwa je jibu hilo linamaanisha ndio au hapana, Keane alisema: “Chukulia unavyopenda.” Na kutimka toka chumba cha mahojiano.
Fergie: “Refa Wiley hayuko fiti!”
Sir Alex Ferguson amemshambulia Refa Alan Wiley aliechezesha mechi ya jana iliyoisha 2-2 kati ya Timu yake Manchester United na Sunderland kwenye Ligi Kuu na kunusurika kufungwa kwa kusawazisha kwa bao la kujifunga mwenyewe kwa Beki Anton Ferdinand katika dakika za majeruhi.
Ferguson amedai Wiley hakuongeza muda sahihi kwenye dakika za majeruhi kwa vile hakuhesabu muda mpira uliposimama baada ya Man U kusawazisha na kuacha muda ubaki dakika zilezile 4 zilizoonyeshwa baada ya dakika 90 kwisha.
Goli la Man U la kusawazisha lilifungwa katika dakika hizo 4 za nyongeza.
Ferguson alisema: “Refa amenisikitisha. Hakuongeza muda wowote juu ya dakika zile 4 ingawa mpira ulisimama tulipofunga ndani ya dakika hizo 4. Alikuwa akitembea uwanjani badala ya kukimbia. Dhahiri alionyesha hayuko fiti. Kasi ya mchezo ilitaka Refa aliefiti. Angalia Marefa wa nje. Wako fiti kam Mbwa wa mwenye Bucha! Refa alikuwa akichukua sekunde 30 kumpa Mchezaji Kadi na kumwandika! Bila shaka alikuwa akipumzika wakati huo!”
Hata hivyo, Ferguson alikiri Man U ilicheza mpira mbovu sana na alikerwa na goli la pili walilofungwa. Ferguson alisema: “Ni goli laini! Pasi zetu zilikuwa mbovu! Hatukucheza vizuri!”
MATOKEO LIGI ZA ULAYA:
BUNDESLIGA:
Ijumaa, Oktoba 2:
Schalke 04 2 v Eintracht Frankfurt 0
Jumamosi, Oktoba 3
Bayer 04 Leverkusen 4 v FC Nurnberg 0
Bayern Munich 0 v FC Koln 0
Hannover 5 v SC Freiburg 2
VFL Bochum 1 v VfL Wolfsburg 1
FSV Mainz 2 v TSG Hoffeinheim 1
Borussia Munchen Gldbach 0 v VB Borussia Dortmund 1
ITALIA SERIE A:
Jumamosi, Oktoba 3
As Bari 0 v Catania 0
Inter Milan 2 v Udinese 1
SPAIN LA LIGA:
Jumamosi, Oktoba 3:
Cd Tenerife 0 v Deportivo La Coruna 1
FC Bacerlona 1 v UD Almeria 0
Atletico de Madrid 2 v Real Zaragoza 0
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009
Raundi ya Pili yakamilika!
MATOKEO MECHI ZA JANA:
Costa Rica 2 Czech Republic 3
Australia 1 Brazil 3
Hungary 2 UAE 0
South Africa 2 Honduras 0
RATIBA RAUNDI YA PILI:
Jumatatu Oktoba 5:
Spain v Italy
Paraguay v Korea Republic
Jumanne, Oktoba 6:
Ghana v South Africa
Egypt v Costa Rica
Hungary v Czech Republic
Jumatano, Oktoba 7:
Brazil v Uruguay
Venezuela v UAE
Germany v Nigeria

No comments:

Powered By Blogger