Saturday 10 October 2009

Nahodha wa Italia Cannavaro mashakani!
Kuumwa na Dondola kwamletea kasheshe!!!
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Italia, Fabio Cannavaro, yupo kwenye uchunguzi wa Maafisa wa Madawa yaliyopigwa marufuku baada ya kupimwa na kugundulika alitumia dawa ambayo hairuhusiwi.
Inasemekana Cannavaro aliumwa na Dondola mwezi Agosti na Klabu yake Juventus ikampa dawa ya kuzuia madhara ya Dondola huyo kwa vile hudhurika akiumwa na Wadudu.
Lakini dawa waliyompa ina chembechembe za ‘cortisone’ ambayo ni marufuku kwa Wanamichezo.
Klabu yake Juventus ilimwombea kibali cha kutumia dawa hiyo na wakati ombi hilo bado halijashughulikiwa Wapima Wachezaji wanaocheki utumiaji Madawa Marufuku wakampima Cannavaro na kugundua ukiukwaji huo.
Kamati ya Olimpiki ya Italia inayoshughulikia Madawa kwa Wachezaji imemwita Cannavaro ili ajieleze.
Cannavaro ndie Mchezaji aliechezea Timu ya Taifa ya Italia mechi nyingi na ndie aliekuwa mhimili wa Italia kunyakua Kombe la Dunia mwaka 2006.
Italia leo wako mjini Dublin, Ireland kucheza na Ireland na wanahitaji sare tu ili waingie Fainali huko Afrika Kusini mwakani.

No comments:

Powered By Blogger