Tuesday 16 March 2010

Beckham afanyiwa upasuaji, pengine nje Miezi 6!!
Profesa Sakari Orava, Daktari aliemfanyia operesheni Nyota David Beckham huko Finland kuiunga musuli toka kisiginoni hadi nyuma ya ugoko mguuni, amesema upasuaji huo ulikwenda vizuri na pengine hatacheza mpira kwa muda wa miezi 6.
Beckham aliumia Jumapili akiichezea AC Milan iliyoifunga Chievo.
Hili ni pigo binafsi kwa Beckham kwani nia yake ilikuwa awe Mchezaji wa kwanza toka England aliecheza Fainali za Kombe la Dunia mara 4.
Mpaka sasa Beckham, ambae anashikilia rekodi ya Mchezaji wa mbele aliechezea England mara nyingi akiwa amewakilisha mara 115, amefungana na Mastaa wa zamani Bobby Moore na Kipa Peter Shilton kwa kucheza Fainali 3 za Kombe la Dunia.
Liverpool yaibomoa Kibonde Portsmouth!!!
• Pengine Gerrard kutwangwa rungu na FA!!!
Jana, katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Anfield, Liverpool iliwafumua Portsmouth bao 4-1 na kuendelea kuwadidimiza mkiani.
Mabao matatu ya Kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Torres, Babel na Aquilani na la 4 la Torres tena ndio yaliwapa ushindi Liverpool.
Bao la Portsmouth lilifungwa na Nadir Belhadj.
Hata hivyo huenda Liverpool wakakumbwa na balaa la kupewa adhabu Nahodha wao Steven Gerrard baada ya kamera kumnasa akimpiga kipepsi Mchezaji Michael Brown wa Portsmouth kwenye dakika ya 73.
Refa Stuart Attwell alitoa faulo kwa kosa hilo lakini huenda akaombwa na FA kuliangalia tena tukio hilo kwenye video na atoe maoni yake.
Wiki iliyopita, Gerrard alinusurika rungu la FA baada ya pia kunaswa kwenye kamera akimtukana Refa Andre Marriner na kuonyesha alama ya V kwa vidole lakini Refa huyo alisema aliliona na kuamua ni kosa dogo na ndio maana hakumchukulia hatua yeyote.
LEO LIGI KUU: Wigan v Aston Villa
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu leo usiku saa 4 dakika 45 saa za bongo, Wigan wataikaribisha Aston Villa uwanja wa DW.
Aston Villa wako nafasi ya 7 na wana pointi 46.
Wigan wao wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi 28.
Fergie atabiri mwisho mgumu Ligi Kuu
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametabiri kuwa msimu huu Ligi Kuu England ndio ngumu kuitabiri katika historia ya Ligi hiyo.
Ingawa amekiri Bingwa atatoka kati ya Timu yake, Chelsea au Arsenal, Ferguson amesema: “Ni ngumu kujua nani Bingwa! Tuna mechi 8 zimebaki. Chelsea ana 9. Wote tuna mashindano Ulaya na Chelsea pia yupo kwenye Kombe la FA.”
Ni mara tatu tu Ubingwa wa Ligi Kuu umeamuliwa kwa tofauti ya pointi moja tu na mara ya kwanza ilikuwa pale msimu wa 1994/94 Blackburn Rovers ilipoipiku Man United, ya pili ilikuwa mwaka 1997/98 Arsenal alipoitoa Man United na mwaka 1998/9 Man United wakalipa kisasi kwa Arsenal.
=======================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 30 pointi 66
2. Chelsea mechi 29 pointi 64
3. Arsenal mechi 30 pointi 64
4. Tottenham mechi 29 pointi 52
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
5. Liverpool mechi 30 pointi 51
6. Man City mechi 28 mechi 50
7. Aston Villa mechi 27 pointi 46
8. Birmingham mechi 29 pointi 44
9. Everton mechi 29 pointi 42
10. Fulham mechi 29 pointi mechi 38
11. Stoke mechi 29 pointi 36
12. Blackburn mechi 29 pointi 34
13. Bolton mechi 30 pointi 32
14. Sunderland mechi 29 pointi 31
15. Wigan mechi 29 pointi 28
16. West Ham mechi 29 pointi 27
17. Wolves mechi 29 pointi 27
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 30 pointi 24
19. Hull mechi 29 pointi 24
20. Portsmouth mechi 29 pointi 19
======================================================================
Manchester United, wanaoongoza kwa pointi 2 juu ya Chelsea ambao wana mechi moja mkononi, wana mechi mbili ngumu zinazofuata ingawa zote ni za nyumbani Old Trafford watakapozivaa Liverpool na kisha Chelsea lakini Ferguson amesema: “Ni lazima ufikirie tofauti ya magoli. Sisi tupo mbele kwa goli 4 kwa Chelsea ingawa ningependa ingekuwa 14! Kitu rahisi kufikiria ni kuwa sisi na Chelsea tucheze na kushinda mechi zetu zote lakini maisha si rahisi kiasi hicho!”

No comments:

Powered By Blogger