Monday 15 March 2010

Hull City yamtimua Phil Brown
Timu iliyo ya pili toka mkiani Hull City leo imemwondoa kazini aliekuwa Meneja wao Phil Brown na kutangaza kuwa Wasaidizi wake Brian Horton na Steve Parkin ndio watakaoiongoza Timu hiyo.
Brown alianza kazi Hull City mwaka 2007 na ndani ya msimu mmoja tu akaipandisha Daraja na kuingia Ligi Kuu mwaka 2008 na kuiwezesha kubaki hapo msimu uliopita japo ilibidi isubiri hadi mechi ya mwisho ya Ligi kujihakikishia wanabaki Ligi Kuu.
Msimu huu mambo yameenda vibaya na wakiwa wamebakisha mechi 9 kumalizi Ligi Menejimenti ya Hull imeamua kubadilisha mwelekeo ili kujinusuru.
LEO LIGI KUU: Liverpool v Portsmouth
Ndani ya Anfield, Liverpool leo wanaivaa Timu ya mkiani Portsmouth kwenye mechi ya pekee ya Ligi Kuu.
Kimsimamo, Liverpool wapo nafasi ya 6 wakiwa wamecheza mechi 29 na wana pointi 48 na juu yao wapo Manchester City walio na pointi 50 kwa mechi 28.
Nafasi ya 4 inashikiliwa na Tottenham wenye pointi 52 kwa mechi 29.

No comments:

Powered By Blogger