Thursday 18 March 2010

Droo za UEFA kesho Ijumaa
Droo za Robo Fainali na Nusu Fainali za Mashindano ya UEFA ya CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI zitafanyika Ijumaa Machi 19 huko Makao Makuu ya UEFA Nyon, Uswisi.
Droo hizo mbili zitahusisha Timu 8 katika kila Mashindano hayo mawili na zitakuwa wazi ikimaanisha upo uwezekano wa Timu toka Nchi moja kupambanishwa na hivyo kwenye CHAMPIONS LIGI upo uwezekano Manchester United akakutana na Arsenal.
Katika CHAMPIONS LIGI, Timu hizo 8 ni:
-Arsenal
-Bayern Munich
-Manchester United
-Lyon
-Barcelona
-Bordeaux
-Inter Milan
-CSKA Moscow
Timu 8 za EUROPA LIGI zitakazoingia kwenye Droo zitajulikana baadae leo usiku baada ya mechi za Ligi hiyo za marudiano kukamilika leo.
Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini hapo Machi 30 na 31 na marudiano yake ni Aprili 6 na 7.
Vile vile itafanyika Droo ya Nusu Fainali na hivyo mbali ya kujua Wapinzani wao wa Robo Fainali Timu zitajua nani watakutana nao Nusu Fainali wakipita Robo Fainali.
Nusu Fainali pia zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na mechi za kwanza zitakuwa Aprili 20 na 21 na marudiano ni Aprili 27 na 28.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ni Mei 22 kwenye Uwanja wa Real Madrid Santiago Bernabeu huko Madrid, Spain.
Kwa EUROPA LIGI, Droo yake itakuwa sawa kama CHAMPIONS LIGI na Robo Fainali zitachezwa Aprili 1 na 8 na Nusu Fainali ni Aprili 22 na 29.
Fainali ya EUROPA LIGI ni Mei 12 Uwanja wa Hamburg Arena Mjini Hamburg, Ujerumani.
Mchezaji Liverpool ambatukia Meneja wake!!
Mchezaji wa Liverpool Albert Riera ametoboa kuwa uhusiano wake na Meneja wake Rafa Benitez ambae ni Mhispania mwenzake umezorota kiasi ambacho anahisi Meneja huyo ana chuki binafsi na yeye.
Riera amedai Rafa ni ‘kiziwi’ kwa Wachezaji na ameielezea Timu ya Liverpool kama Meli ‘inayozama’.
Riera ameichezea Liverpool mara mbili toka mwishoni mwa Januari huku akianza mechi moja na nyingine akitokea benchi la akiba.
Riera amesema anafikiria sana kuhama ili ajijengee mazingira mazuri ya kuchukuliwa Kikosi cha Spain cha Kombe la Dunia.
Riera amesema yuko tayari kwenda Urusi kwa vile Soko la Wachezaji huko liko wazi kwa vile msimu wao mpya ndio kwanza umeanza.
Riera amenukuliwa na Radio Marca ya huko Spain akisema: “Kama Kocha hakuambii chochote na wewe uko fiti na unafanya tizi vizuri tu bila shaka utafikiria kuna chuki! Timu inacheza vibaya, mabadiliko yanatakiwa! Kama ninafanya vibaya ni wajibu wa Kocha kuniambia kosa langu ili nijirekebishe! Kinachouma hakwambia kitu na hilo si kwa mimi pekee! Wako Wachezaji wengine pia!”

No comments:

Powered By Blogger