Monday 15 March 2010

BECKHAM: Bai Bai Kombe la Dunia!! Kuwa nje Miezi 4!!
Daktari ambae atamfanyia upasuaji David Beckham amethibitisha kuwa Nyota huyo atakuwa nje ya uwanja hadi miezi minne baada ya kuumia musuli ya mguu inayounganisha kisigino cha mguu na nyuma ya ugoko katika mechi ya Klabu yake ya mkopo AC Milan na Chievo siku ya Jumapili.
Beckham alitegemewa kuwemo kwenye Kikosi cha Timu ya England kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia linaloanza Juni 11 lakini Dokta Sakari Orava ambae ndie atafanya upasuaji ili kumuunga musuli hiyo iliyokatika alisema itachukua miezi mitatu ili aweze kupona na kuanza tena mazoezi na muda wa mwezi mmoja zaidi unatakiwa ili kumweka fiti tena.
Hali hiyo inamaanisha Beckham hawezi kupona kwa wakati ili kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Mourinho: “Mourinho hafungwi Stamford Bridge!!!”
Ballack: “Mourinho ni historia! Tuna njaa ya Ubingwa Ulaya!”
Jose Mourinho ana matumaini makubwa ya kurudi tena Uwanja wa Stamford Bridge kwa furaha na amedai Mourinho hafungiki Stamford Bridge.
Mourinho alikuwa Kocha wa Chelsea kuanzia 2004 hadi 2007 na alitwaa Vikombe kadhaa na pia kuifanya Stamford Bridge iwe ngome isiyofungika ya Chelsea.
Mourinho atakuwa na Timu yake ya sasa Inter Milan itakayokwaana na Chelsea kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI hapo Jumanne hii ikiwa ni mechi ya marudio.
Inter Milan iliibwaga Chelsea 2-1 katika mechi ya kwanza.
Jose Mourinho alijigamba: “Kila mtu anajua Mourinho hafungiki Stamford Bridge! Rekodi yangu hapo nlipokuwa na Chelsea kila mtu anaijua!”
Hata hivyo Kiungo wa Chelsea, Mjerumani Michael Ballack, amempinga kwa kudai Mouronhi sasa ni historia tu na wao wana njaa kubwa ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya.
LIGI KUU England: MATOKEO
Jumamosi, Machi 13
Tottenham 3 v Blackburn 1
Birmingham 2 v Everton 2
Bolton 4 v Wigan 0
Burnley 1 v Wolves 2
Chelsea 4 v West Ham 1
Stoke 0 v Aston Villa 0
Hull 1 v Arsenal 2
Jumapili, Machi 14
Man United 3 v Fulham 0
Sunderland 1 v Man City 1

No comments:

Powered By Blogger