Wednesday 17 March 2010

Pompey wakatwa pointi 9!!!
Kushuka Daraja ni uhakika!!!
Klabu iliyo kwenye matatizo makubwa kifedha na ambayo pia ipo mkiani mwa Ligi Kuu, Portsmouth, leo imekatwa pointi 9 na Ligi Kuu kwa kukiuka taratibu za Ligi Kuu baada ya kukabidhiwa kwa Msimamizi maalum ili kuinusuru isifilisiwe.
Hatua hiyo ya Ligi Kuu inafuatia Mahakama Kuu kuamua hapo jana kuwa Msimamizi huyo ni halali na hivyo Klabu hiyo isifilisiwe na Mamlaka ya Kodi waliotaka amri ya kufilisiwa itolewa kwa Klabu hiyo baada ya kushindwa kulipa kodi.
Wasimamizi wa Ligi Kuu wamethibitisha hatua ya Portsmouth kukatwa pointi 9 na hivyo kubakishwa na pointi 10 tu na sasa wako nyuma ya Timu za 18 na 19 kwenye msimamo Hull City na Burnley kwa pointi 14.
Hatua hiyo ya Ligi Kuu, bila shaka, itaiporomosha Daraja Portsmouth kwani wamebakiza mechi 9 tu.
Hull City yamteua Dowie Meneja mpya!!
Meneja wa zamani wa Crystal Palace, Ian Dowie, ametajwa kuwa ndie Meneja mpya wa Hull City kuchukua nafasi ya Phil Brown aliefukuzwa majuzi.
Dowie ameletwa hapo mahsusi ili kuinusuru Hull City isiporomoke Daraja kutoka Ligi Kuu.
Hull ipo nafasi moja toka mkiani ikiwa na pointi 24 na imebakisha mechi 9.
Msimu uliokwisha Hull ilinusurika kushushwa kwenye mechi ya mwisho ya Ligi.
Terry amgonga na gari Mlinzi wao Stamford Bridge!!
Kuna ripoti kuwa Nahodha wa Chelsea John Terry amemvunja mguu Mlinzi wa Chelsea wa Uwanjani Stamford Bridge kwa gari lake mara baada ya mechi ya jana usiku ambayo Chelsea walifungwa 1-0 na Inter Milan na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Inasemekana wakati Terry akiondoka Uwanjani hapo gari lake likiwa kwenye msongamano wa magari na mwendo wa polepole huku likizongwa na Washabiki na Waandishi wa Habari Mlinzi huyo alianguka na ndipo akavunjwa mguu na gari la Terry.
Inadaiwa Terry ametoa pole kwa Mlinzi huyo na Polisi wanachunguza tukio hilo.

No comments:

Powered By Blogger