Saturday, 20 March 2010

LIGI KUU: Mechi za Jumamosi na Jumapili
RATIBA:
[saa za bongo]
Jumamosi, Machi 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Aston Villa v Wolves
[saa 12 jioni]
Everton v Bolton
Portsmouth v Hull
Stoke v Tottenham
Sunderland v Birmingham
Wigan v Burnley
[saa 2 na nusu usiku]
Arsenal v West Ham
Jumapili, Machi 21
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Liverpool
[saa 12 jioni]
Fulham v Man City
[saa 1 usiku]
Blackburn v Chelsea
=========================================================================
MSIMAMO LIGI KUU England:
1. Man United mechi 30 pointi 66
2. Chelsea mechi 29 pointi 64
3. Arsenal mechi 30 pointi 64
4. Tottenham mechi 29 pointi 52
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
5. Liverpool mechi 30 pointi 51
6. Man City mechi 28 mechi 50
7. Aston Villa mechi 28 pointi 49
8. Birmingham mechi 29 pointi 44
9. Everton mechi 29 pointi 42
10. Fulham mechi 29 pointi mechi 38
11. Stoke mechi 29 pointi 36
12. Blackburn mechi 29 pointi 34
13. Bolton mechi 30 pointi 32
14. Sunderland mechi 29 pointi 31
15. Wigan mechi 30 pointi 28
16. West Ham mechi 29 pointi 27
17. Wolves mechi 29 pointi 27
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
18. Burnley mechi 30 pointi 24
19. Hull mechi 29 pointi 24
20. Portsmouth mechi 29 pointi 10
========================================================================
UCHAMBUZI:
BIGI MECHI: Manchester United v Liverpool [Jumapili, Old Trafford]
Bila shaka, BIGI MECHI ni Jumapili huko Old Trafford kati ya Mahasimu wakubwa Manchester United, wanaoongoza Ligi na wanaotafuta Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo ikiwa ni rekodi na pia kuwapiku Liverpool kwa kuchukua Ubingwa kwa mara ya 19, watakapowavaa Liverpool, Timu inayosuasua Msimu huu na huenda wakaikosa hata nafasi ya 4 na hivyo kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI msimu ujao.
Aston Villa v Wolves
Hii ndio mechi ya fungua dimba wikiendi hii na itachezwa saa 9 dakika 45, saa za bongo, huku Villa wakiwania nafasi ya 4 inayogombewa sana kwa vile itaifanikisha Timu itakayoitwaa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI hasa kwa vile nafasi 3 za juu za Ligi zimeshahodhiwa na Man United, Chelsea na Arsenal.
Villa wako pointi 3 nyuma ya Tottenham walio nafasi ya 4 lakini Villa wana mechi moja mkononi.
Wolves wanaingia mechi hii wakitoka kwenye ushindi wa nadra wa ugenini walipoifunga Burnley 2-1 mechi iliyokwisha.
Portsmouth v Hull City
Hii ni mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Hull City, Ian Dowie.
Kwa Portsmouth, baada ya kukatwa pointi 9, kuporomoka Daraja ndio njia pekee kwao kwani sasa wana pointi 10 tu, wamebakisha mechi 9 na Timu iliyo juu yao iko mbele kwa pointi 14.
Kilichobaki kwao ni kucheza kulinda fahari yao.
Arsenal v West Ham United
Kwa vile Man United na Chelsea zote zinacheza Jumapili, ushindi kwa Arsenal utawafanya waongoze Ligi lakini hii ni dabi ya Timu za London na huwa haitabiriki.
Katika mechi iliyokwisha, Arsenal walipata ushindi dakika za majeruhi pale Nicklas Bendtner alipowafungia bao la pili dhidi ya Hull City.
West Ham wapo kwenye majaribuni makubwa baada ya kupoteza mechi 3 za mwisho na wako nafasi ya 16 kwenye Ligi.
Stoke City v Tottenham Hotspur
Hii ni tripu ngumu kwa Tottenham walio nafasi ya 4 watakapokuwa wageni wa Stoke Uwanjani Britannia ambako Stoke wamefungwa mechi moja tu ya Ligi Kuu katika 10 zilizochezwa uwanjani hapo.
Tottenham pia watakumbuka walipokuwa kwao White Hart Lane walifungwa na Stoke kwenye mechi ya kwanza ya Ligi.
Wigan v Burnley
Hii ni vita ya Timu zinazopigana kukimbia kuporomoka Daraja na zimetenganishwa na pointi 4 huku Burnley wakiwa moja ya Timu 3 zilizo nafasi za mwisho na hivyo eneo la kushuka Daraja.
Sunderland v Birmingham
Baada ya kucheza mechi 14 bila ushindi, Sunderland wameweza kupata pointi 5 katika mechi zao 3 za mwisho za Ligi na ushindi mwingine utawafanya Sunderland walikimbie lile eneo la hatari la kuporomoka Daraja.
Birmingham wao wako nafasi ya 8 na ni Timu iliyo na matokeo mazuri kwa jumla.
Everton v Bolton Wanderers
Ndani ya Goodison Park, Everton wanawakaribisha Bolton ambao walishinda kwa kishindo mechi yao iliyokwisha walipoitwanga Wigan 4-0 na hivyo kujiwekea tofauti ya pointi 8 na Timu zilizo hatarini kuteremka Daraja.
Everton, waloanza vibaya msimu huu, wameibuka mwaka huu 2010 na kuwa na matokeo mazuri na kuwafanya wawe nafasi ya 9.
Fulham v Manchester City
Jumapili, Uwanja wa Crave Cottage utawakutanisha wenyeji Fulham na Man City huku Fulham wakitoka kwenye furaha ya kuwanyuka 4-0 Vigogo wa Italia Juventus na kutinga Robo Fainali ya EUROPA LIGI ambako watacheza na Wolfsburg ya Ujerumani.
Fulham wakiwa nyumbani ni wagumu kwani wamepoteza mechi moja tu katika 11 lakini Man City ni goigoi wakisafiri na wameshinda mechi 2 tu katika 13.
Blackburn Rovers v Chelsea
Wakiwa nyumbani Ewood Park siku ya Jumapili, Blackburn watakutana na Chelsea waliotunguliwa na Meneja wao wa zamani Jose Mourinho na Inter Milan yake na hivyo kubwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Chelsea huwa mara nyingi wanasumbuka kushinda ugenini msimu huu na Blackburn ni wagumu mno kufungika kwao na wameshinda mechi zao 4 za mwisho.

No comments:

Powered By Blogger