Friday 19 March 2010

Refa afungiwa maisha!!!
UEFA imempa Refa Oleh Orekhov kutoka Ukraine kifungo cha maisha katika masuala ya Soka kutokana na kuhusika na upangaji matokeo wa mechi.
UEFA imetamka kuwa Refa huyo alikiuka misingi ya uaminifu na maadili ya kandanda lakini haikutaja ni Ligi ipi au mechi zipi Refa huyo alipanga matokeo.
Taarifa hiyo ya UEFA imesema uamuzi wao unatokana na fununu walizopewa na Polisi wa Ujerumani waliokuwa wakichunguza zaidi ya mechi 200 zilizochezwa katika Nchi 11 ambazo zilikuwa zimegubikwa na utata wa upangaji matokeo.
Uamuzi huo wa UEFA umetoka kwenye Bodi yao ya Nidhamu na Udhibiti ambayo maamuzi yake yanaweza kukatiwa Rufaa ndani ya siku 3 baada ya Mtuhumiwa kupokea rasmi taarifa ya adhabu yake.
LIGI KUU England: RATIBA Wikiendi hii
[saa za bongo]
Jumamosi, Machi 20
[saa 9 dak 45 mchana]
Aston Villa v Wolves
[saa 12 jioni]
Everton v Bolton
Portsmouth v Hull
Stoke v Tottenham
Sunderland v Birmingham
Wigan v Burnley
[saa 2 na nusu usiku]
Arsenal v West Ham
Jumapili, Machi 21
[saa 10 na nusu jioni]
Man United v Liverpool
[saa 12 jioni]
Fulham v Man City
[saa 1 usiku]
Blackburn v Chelsea
Beckham kupewa wadhifa Timu ya England huko Bondeni
Huenda David Beckham, alieumia na hivyo hatoweza kuichezea England Fainali za Kombe la Dunia, akapewa wadhifa ili awe mmoja wa Maafisa wa Kikosi cha England kitakachokwenda Afrika Kusini kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Kabla ya kuumia na kufanyiwa opersheni Nchini Finland Jumatatu iliyopita, David Beckham alitegemewa kuwa mmoja wa Wachezaji wa England na kwa vile hawezi kucheza Kocha wa England Fabio Capello anategemewa kumchukua Beckham kama mmoja wa Viongozi ili kuipa morali Timu hasa kwa vile Wachezaji wengi wanampenda na kumheshimu.
Wakati huohuo, David Beckham ametoa shukrani zake kwa Madaktari wa huko Finland pamoja na Watu wote waliomtakia heri.

No comments:

Powered By Blogger