Thursday 4 June 2009

Bongo 2 New Zealand 1
Jana Taifa Stars waliifunga New Zealand mabao 2-1 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
New Zealand wako njiani kwenda Afrika Kusini kushiriki Kombe la Mabara la FIFA litakaloanza Juni 14 na kushirikisha Nchi Bingwa wa Mabara yote Duniani pamoja na Mwenyeji Afrika Kusini na Bingwa wa Dunia Italia. Nchi nyingine kwenye Mashindano hayo ya FIFA ya kuwapa uhondo Washabiki kabla ya Fainali Kombe la Dunia mwakani ni Brazil, Egypt, Spain, USA na Iraq
Mabao ya Bongo yalifungwa na Jerry Tegete na Mwinyi Kazimoto.
Baada ya mechi, Kocha wa New Zealand aliipa bigi faivu Stars kwa mchezo murua na kusema Tanzania imepanda kisoka.
Nae Maximo, Kocha wa Bongo, alifurahishwa na bidii za Wachezaji wake na kuwataka wasilegeze uzi katika mazoezi.
Ufaransa yafungwa na Nigeria na kuzomewa!!!
Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech amelalamika baada ya Wachezaji wa Ufaransa kuzomewa na Mashabiki katika mechi ya kirafiki na Nigeria waliyotunguliwa bao 1-0 hapo juzi.
Domenech amevisema vitendo hivyo ni ubaguzi kwa vile vililenga kwa baadhi ya Wachezaji hasa Wachezaji wanaochezea Lyon kwa vile mechi ilichezwa Uwanja wa Klabu ya St Etienne ambayo ni pinzani na Lyon.
Wachezaji Karim Benzema na Sidney Govou, wote wa Lyon, ndio waliozomewa mno na Mashabiki hao na Domenech, ambae zamani alikuwa Mchezaji wa Lyon, amekiita kitendo hicho ni usaliti na ubaguzi mkubwa.
Ufaransa wanacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Uturuki Ijumaa kwenye Uwanja wa Lyon kwani mechi zao za mchujo kuingia Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 mwezi Agosti watakapocheza na Faroe Islands na Septemba watacheza na Romania.

1 comment:

Anonymous said...

WANATUMIA VUDU, NGUVU ZA GIZA BILA HIVYO HANA KITU.

Powered By Blogger