Saturday 12 September 2009

Adebayor atoboa nini ugomvi wake na Bendtner!!!
Kisa ni viatu!!!
Januari 22, 2008, kwenye mechi ya Kombe la Carling, ulimwengu wa soka ulipigwa butaa baada ya kushuhudia Wachezaji wa Timu moja wakigombana na mmoja kumtwanga kichwa mwenziwe na kumpasua.
Tukio hilo liliihusu Arsenal walipocheza na Tottenham na Wachezaji hao ni Emmanuel Adebayor alipomvisha mwenziwe Nicklas Bendtner ‘ndoo!”
Wakati leo Adebayor na Bendtner watakutana uso kwa uso, safari hii wakiwa Timu pinzani, Adebayor akiwa Manchester City na Nicklas Bendtner akiwa bado yuko Arsenal, Adebayor ametoa bayana nini chanzo cha ugomvi huo.
Adebayor ametoboa kuwa mwanzo kabisa wa mfarakano wao ni viatu!
Adebayor amesema Klabuni Arsenal kulikuwa na sheria kuwa Mchezaji yeyote haruhusiwi kuingia kwenye Chumba cha kubadilishia Jezi na viatu vyake binafsi vya nyumbani.
Adebayor akapasua: “Kila siku Bendtner alivunja sheria hiyo na kuingia Chumbani humo na viatu vyake binafsi vya nyumbani! Nikamwambia tuheshimiane na vua viatu! Hapo ndipo uhasama ukaanza!”
Kuhusu siku aliyompiga kichwa Bendtner kwenye mechi, Adebayor ameeleza: “Alininyooshea kidole! Huwezi kumnyooshea mtu kidole!”
Kuhusu mechi ya leo kati ya Man City na Arsenal, Adebayor amesema: “Naiheshimu Arsenal na namuheshimu Wenger kama Meneja! Alex Song na Emmanuel Eboue sio marafiki- ni ndugu! Tumefanya vitu vingi pamoja na wao! Lakini sasa niko Man City na wao si marafiki wa Man City! Sasa leo kati ya saa 11 na saa 1 tutakuwa si ndugu! Baada ya mechi udugu utarudi!”
Na Bendtner je? Bila shaka uhasama wa viatu unaendelea!

No comments:

Powered By Blogger