Saturday 12 September 2009

Mjomba wa Berbatov alikuwa na wasiwasi kwake kujiunga na “Mashetani Wekundu!”
Mjomba wake Dimitar Berbatov ambae ni Padri anaepunga watu Mashetani alipatwa na wasiwasi mkubwa na kumkataza asijiunge na “Mashetani Wekundu!”
Berbatov anasema: “Mjomba wangu huko kwetu Bulgaria ni Padre anaepunga watu Mashetani na kufukuza pepo mbaya sasa aliposikia najiunga na Manchester United ambao jina la utani ni “Mashetani Wekundu” alinikataza nisifuate Mashetani!”
Lakini baadae, Mjomba huyo huyo, amemshukuru Berbatov kwa kuihama Tottenham na kwenda Manchester United na Berbatov anasema: “Ameniambia Kanisa lake limepata Waumini wengi zaidi! Bulgaria watu ni wehu kwa mpira na sasa Kanisa linajaa kwa vile nipo Manchester United! Lakini, kitu kizuri ni kuwa wanaenda huko kusikiliza na kujifunza kutoka kwa Padre!”
Kwa Berbatov, ingawa kwa sasa ni tajiri na mtu maarufu sana, Familia yake inabaki muhimu sana kwake na mwenyewe anadai aliamua kuihama Tottenham kwenda Man U alipokuwa akilima kabeji na viazi bustanini kwa Babu yake na ndipo Babu yake huyo akamshauri ajiunge na Man U.
Berbatov anasema: “Mafaninkio yangu ni kwa sababu ya Mama yangu. Sala zake, upendo wake na msaada wake ndio umenifikisha hapa! Najua hata nikimfanyia kitu chochte kikubwa hakiwezi kulipa msaada wake! Babu na Bibi yangu ni watu muhimu pia! Nikiwa likizo huwa nakuwa bustanini kwa Babu na yeye ni mtu mwenye hekima sana! Tunalima na ananipa mawaidha na ni yeye alieniambia nijiunge na Man U!”
Leo jioni, Berbatov anarudi uwanjani White Hart Lane nyumbani kwa Klabu yake ya zamani Tottenham na ametamka: “Nilifurahia wakati wangu nilipokuwa Spurs na Mashabiki walinipenda! Lakini ukisikia Klabu kama Man U inakutaka na unapata nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE, haiwezekani ukasema hapana!”

No comments:

Powered By Blogger