Bilic adai wamegundua udhaifu wa England!
Kocha wa Croatia, Slaven Bilic, ambayo Timu yake inakutana na England Jumatano Uwanjani Wembley kwenye mechi muhimu ya mtoano ya kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia, amedai kuwa wamegundua udhaifu wa Timu ya England na watatumia mwanya huo siku hiyo ya Jumatano.
Mpaka sasa, England, walio chini ya Kocha toka Italia, Fabio Capello, wanaongoza Kundi lao kwa kushinda mechi 7 katika 7 walizocheza na wako mbele ya timu ya pili Croatia kwa pointi 4 na pia wana mechi moja mkononi.
England wakiifunga Croatia hiyo Jumatano watatinga Fainali Afrika Kusini.
Croatia, walio nafasi ya pili Kundi hili, wamewazidi Timu ya 3, Ukraine, pointi 3 lakini Ukraine wana mechi moja mkononi.
Hivyo, ni muhimu sana Croatia kuifunga England ingawa itakuwa mechi ngumu kwao hasa kwa vile katika mechi ya kwanza kati ya timu hizo, England waliwaumbua Croatia kwa kuwapigia bao 4-1 nyumbani kwao mjni Zagreb.
Hata hivyo, Croatia wanapata matumaini hasa wakikumbuka Novemba, 2007, Uwanjani Wembley, walipowafunga England 3-2 na kuwang’oa England kuingia Fainali za EURO 2008.
Slaven Bilic, enzi za Uchezaji wake alichezea West Ham mwaka 1996 na 1997 kisha kwenda kucheza Everton mwaka 1997 hadi 2000, amesema: “England kwa sasa ni Timu tofauti. Wana uzuri wao lakini kuna kitu kimepungua kwao. Sasa wanaukosa ule “Uingereza” ambao uliifanya iwe ngumu kufungika zamani! Lakini, tunajua nini hasa wanakikosa na siwezi kuwaambia ni nini! Ni siri yetu!”
No comments:
Post a Comment