Thursday, 10 September 2009

England, Spain zabingiria Bondeni!!
Mashine za Germany, Italia zanguruma kuelekea Bondeni!!
Ufaransa bado kimbembe!!
England waliitandika Croatia mabao 5-1 Uwanjani Wembley na kutinga Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini.
Mabao ya England yalifungwa na Frank Lampard, bao 2, Steven Gerrard, 2, na Wayne Rooney. Bao la Croatia lilifungwa na Eduardo.
Spain nao waliwapiga Estonia mabao 3-0 na wapinzani wao Bosnia-Herzegovina na Uturuki kutoka suluhu na hivyo kuwapa mwanya Spain kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia.

Mambo kwa Ufaransa ni magumu kwani jana wakiwa ugenini walitoka suluhu 1-1 na Serbia ambao wanaongoza Kundi lao kwa pointi 4 mbele ya Ufaransa huku mechi zimebaki 2.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA ULAYA ZA JANA:
Jumatano, 9 Septemba 2009
Albania 1 v Denmark 1,
Andorra 1 v Kazakhstan 3,
Armenia 2 v Belgium 1,
Belarus 0 v Ukraine 0,
Bosnia-Herzegovina 1 v Turkey 1,
Czech Republic 7 v San Marino 0,
England 5 v Croatia 0,
Faroe Islands 2 v Lithuania 1,
Germany 4 v Azerbaijan 0,
Hungary 0 v Portugal 1,
Israel 7 v Luxembourg 0,
Italy 2 v Bulgaria 0,
Latvia 2 v Switzerland 2,
Liechtenstein 1 v Finland 1,
Malta 0 v Sweden 1,
Moldova 1 v Greece 1,
Montenegro 1 v Cyprus 1,
Northern Ireland 0 v Slovakia 2,
Norway 2 v FYR Macedonia 1,
Romania 1 v Austria 1,
Scotland 0 v Netherlands 1,
Serbia 1 v France 1,
Slovenia 3 v Poland 0,
Spain 3 v Estonia 0,
Wales 1 v Russia 3,

KOMBE LA DUNIA ASIA: Bahrain yaitoa Saudi Arabia, kupambana na New Zealand na mshindi ataenda Bondeni!!
Jana, Kisiwa kidogo cha Bahrain kiliwatoa Saudi Arabia nishai wakiwa nyumbani kwa kulazimisha suluhu ya 2-2 na kusonga mbele kwa magoli ya ugenini, baada ya mechi ya kwanza huko Bahrain kuwa 0-0 Jumamosi iliyopita, na hivyo mwezi ujao watacheza na New Zealand ili kupata mshindi atakaenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010.
Saudi Arabia walipata bao la pili dakika za majeruhi, dakika ya 94, na kuongoza 2-1 na huku uwanja mzima ukishanglia ushindi wao mkubwa, Bahrain walipata kona na kusawazisha na mechi ikaisha sekunde chache baadae ikiuacha uwanja mzima umepigwa butaa kwani furaha ndani ya sekunde iligeuka huzuni.
Man U yaja juu, yasema hatuwezi kukaa kimya tukitukanwa!!
Mkurugenzi Mkuu wa Manchester United, David Gill, amesema ni ‘matusi’ kuambiwa kuwa wametoa pesa kwa Wazazi wa Paul Pogba ili wamsaini.
Mara baada ya Chelsea kufungiwa na FIFA kusaini wachezaji hadi 2011 kwa kumchukua kinyume cha taratibu Chipukizi Gael Kakuta aiekuwa Klabu ya FC Lens ya Ufaransa, Le Havre nayo pia ya Ufaransa ikaibuka na madai kama hayo wakidai wameporwa Kijana wao Pogba kinyume cha taratibu.
Gill amesema: “Hatuwatishi lakini hatukubali jina zuri la Manchester United lichafuliwe. Sisi tumefuata sheria zote.”
Jumatatu, Man U ilitoa onyo kwa Le Havre kwamba itawashitaki wakiendelea kutoa madai yao.

No comments:

Powered By Blogger