Thursday 10 September 2009

Sweden wapendekeza Wachezaji wasipeane mikono ili kujikinga na Homa ya Mafua ya ‘KITI MOTO’!!!
Chama cha Soka cha Sweden kimetoa pendekezo Wachezaji wasipeane mikono kabla na baada ya mechi ili iwe kinga ya kutoeneza ugonjwa wa Mafua ya ‘Kiti moto’.
Huko Sweden kuliripotiwa Wachezaji kadhaa wa Timu moja waliugua ugonjwa huo ingawa hawakuwa wanatoka Klabu kubwa na wote inasemekana walipona.
Mwezi Julai Mchezaji wa Manchester City, Micah Richards, aliupata ugonjwa huo alipokuwa vakesheni nje ya Uingereza lakini akapona baada ya kupata matibabu na kukaa karantini siku kadhaa.
Mwezi Mei, Klabu za Mexico, Chivas Guadalajara na San Luis, ilibidi zijitoe kwenye Kombe la Klabu za Marekani ya Kusini, Copa Libertadores, baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa huo huko Mexico.

No comments:

Powered By Blogger