Friday 11 September 2009

Germany Mabingwa Ulaya kwa Mabibi!!
Waitandika England 6-2 Fainali ya UEFA!!
Jana huko Helsinki, Finland, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Germany iliwapiga England mabao 6-2 na kunyakua Ubingwa wa Ulaya hii ikiwa ni mara yao ya 5 kuchukua Ubingwa huo.
Ujerumani ilikuwa ya kwanza kupata mabao ya haraka haraka yaliyofungwa na Prinz dakika ya 20 na Behringer dakika ya 22.
England wakakomboa moja dakika ya 24 likifungwa na Carney.
Kipindi cha pili ndipo mvua ya magoli ikaanguka na Germany wakapachika bao la 3 dakika ya 51kupitia Kulig na England wakafunga bao lao la pili na la mwisho dakika ya 55 Mfungaji akiwa Smith.
Germany wakaongeza bao 3 nyingine kupitia Grings, dakika ya 62 na 73, na Prinz akapachika bao lake la pili na la 6 kwa Germany dakika ya 76.

No comments:

Powered By Blogger