Tuesday 8 September 2009

Kipa Paddy Kenny afungiwa Miezi 9 kwa kutumia madawa!!
Kipa wa Sheffield United inayocheza Daraja la Championship, chini tu ya Ligi Kuu, Paddy Kenny, miaka 31, amefungiwa kutocheza soka kwa miezi 9 kuanzia Julai 22, 2009 kwa kupatikana na hatia ya kutumia dawa ‘Ephedrine’ ambayo ipo kwenye listi ya dawa zinazokatazwa kwa Wanasoka kwani huongeza nguvu.
Paddy Kenny aligundulika kutumia dawa hiyo ambayo kawaida hutumika kutibu kifua hasa afueni kwenye pumu katika mechi Sheffield United walipocheza na Preston kwenye mechi maalum za mtoano kutafuta Timu kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu.
Paddy Kenny amekiri kutumia dawa hiyo lakini alijitetea kuwa alikuwa akiumwa kifua.
Kamati ya Sheria ya FA, Chama cha Soka England, imesema imeridhika na utetezi wa Kenny Paddy kuwa hakutumia ‘Ephedrine’ kuongeza nguvu na ndio maana hawakumpa adhabu kali ya kifungo cha miaka miwili lakini ni wajibu wao kutoa adhabu ili iwe fundisho kwa Wachezaji wa Kulipwa kutotumia dawa bila ya maelekezo ya Madaktari wa Klabu zao.
Klabu ya Sheffield United imelalamika kuwa Kamati hiyo kwa sababu imekubali Kipa huyo hakutumia dawa hiyo kuongeza nguvu walitegemea adhabu ndogo zaidi au onyo au msamaha.

No comments:

Powered By Blogger