Tuesday 9 March 2010

England yanaswa kwenye mkanda wa siri!!
Zimeibuka habari kuwa kuna mkanda wa siri umenaswa ukiwa na rekodi ya mazungumzo kati ya Makocha wa England na Wachezaji wao wakiwa hotelini kabla ya mechi ya kirafiki na Misri Jumatano iliyopita.
Mkanda huo uliorekodiwa haujulikana kama ulinaswa kupitia simu au vinasa sauti na umekuwa ukipelekwa kwa Vyombo vingi vya Habari ili ununuliwe.
Lakini Wanasheria wa Timu ya England wamevionya kuwa kuutumia mkanda huo uliorekodiwa kinyume cha sheria ni makosa.
England hivi karibuni iligubikwa na kashfa iliyomhusu John Terry ambae ilimfanya avuliwe Unahodha wa England.
Gerrard huenda akalikwaa rungu la FA!!
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, huenda akajikuta yuko matatani na FA baada ya kunaswa kwenye video akimtukana Refa Andre Marriner na pia kutoa ishara ya V katika mechi ya jana Liverpool waliyofungwa 1-0 na Wigan.
Vitendo hivyo vya Gerrard vilitokea dakika ya 81 baada ya kulambwa Kadi ya Njano na Refa Marriner alipomkwatua kwa nyuma Mchezaji wa Wigan James McCarthy.
Refa Marriner hakuviona vitendo vya Gerrard lakini FA huenda wakaamua kumshitaki Gerrard kwa uhuni.
Rooney afanya mazoezi
Supastaa Straika wa Manchester United Wayne Rooney ameipa nguvu Timu yake baada ya kuonekana akifanya mazoezi na wenzake kwenye Kambi ya mazoezi ya Carrington na huenda akacheza kesho kwenye mechi ya marudiano na AC Milan ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Man United iliifunga AC Milan 3-2 huko San Sirro.
Rooney aliikosa mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi Man United walipoifunga Wolves 1-0 na ilitangazwa ana matatizo ya goti.
Katika mazoezi hayo ya huko Carrington ambacho ndicho kituo cha mazoezi cha Manchester United, Veterani Ryan Giggs alionekana pia akifanya mazoezi.
Giggs alivunjika mkono kwenye mechi ya Ligi Kuu na Aston Villa mwezi uliokwisha.

No comments:

Powered By Blogger